Recent Comments

NGARA TUNATAKA KUSIKIA TAMKO LA CHAMA JE MITANO TENA IPO KWA MADIWANI NA WABUNGE AU HAIPO?

By Mwafrika Jul 5, 2024

Na mwafrika

Kwa kipindi Cha hivi karibuni katika Wilaya ya Ngara pameibuka msneno ya hapa na pale ya kwamba Mbunge aliyepo madarakani Apewe m5 tena na kufikia hatua ya kusema anatosha 2025 ni yeye na SI mwingine.

Nauliza Swali JE ni msiamamo wa Chama? Wananchi?Wanachama?au ni msiamamo wa nani?na kama ni msiamamo wa Chama watu wanatakiwa waambiwe,kama ni msiamamo wa wananchama pia watu wanatakiwa wajue maana nchi yetu inaendeshwa na Demokrasia ya uwepo wa vyama vingi.

Kama tayari watu wanasema Mbunge ni yeye anatosha na hakuna haja ya wengine kuchukua fomu ama hakuna haja ya wananchi kupiga kura Kwa sababu unawezaje kupiga kura Kwa mtu ambae ametosha kabla ya Uchaguzi?

JE vyama vya Upinzani Wilayani Ngara vinasemaje kuhusu wao na hao wengine eanaotosha kuongoza Ngara peke Yao?JE Kama ni kweli anatosha yeye Kuna haja yeyote Ile ya kufanya uchaguzi na Kampeni?maana kama ni yeye tu basi hizo pesa za Kampeni na uchaguzi Ngara zipelekwe mapema Shule hasa pale kanazi ambapo Kuna Shule ya Msingi haina madawati.

Maoni yangu kama ni msimamo wa mtu mmoja basi tupuuze ila kama Kuna haja ya kutoa TAMKO basi toeni mapema Ili watu wakichukua fomu na kukosa wajue wamekosa kihalali na sio kimya ambacho watu watahisi Kuna kamchezo ka mapema.

Ni ushauri tu mkitaka chukueni na msipotaka acheni ila Naeashauri Upinzani wa Ngara na nyie kama mmerizia Ni yeye tu basi hakuna haja ya kufanya Kampeni na msipewe pesa za uchaguzi au mkipewa pelekeni kwenye maendeleo ya nchi.