Recent Comments

WATANZANIA WANAVUNA WANACHO KIPANDA

By Simamia Ngara Jul 6, 2024

NA, ANKO G

Malalamiko ya watanzania juu ya maisha ni mavuno ya aina ya wanasiasa wanao penda kuwachagua hususa ni Wabunge.

Ikumbukwe kuwa siasa ni maisha ya kila siku na mfumo wa serikali ya Tanzania ulivyo maisha yanapangwa na wanasiasa hususa ni wabunge ambapo bunge ni mhimili mojawapo wa serikali na bunge ndilo hutumika kutunga sheria,Kanuni na Kujadili mambo mbalimbali ya kitaifa, Kujadili na kupitisha bajeti pamoja na kuishauri au kuikosoa serikali.

Watanzania ni wasahaulifu sana na wenye kurudia makosa kila baada ya miaka mitano na huu umekua ugonjwa wa kurithi kizazi mpaka kizazi.

Unapo karibia uchaguzi basi utasikia fulani atashinda nafasi fulani kwasababu anapesa nyingi kuwazidi kina fulani na anahonga kuliko kina fulani hivyo fulani hata kama ni mzuri hawezi kushinda kwasababu fulani anapesa za kuhonga ili aweze kushinda nafasi fulani hasa.

Kwa tafsiri nyingine hiyo ni kuuza haki kwa wenye fedha huku wakitarajia k
Viongozi wanao pata nafasi kwa Rushwa waweze kuwa viongozi wazuri na wazalendo wa kuwatetea haki za wananchi

Lazima tukubaliane kwamba ukila lazima uliwe hivyo wanasiasa wengi wanapo chaguliwa na kupita kwa Kutoa Rushwa hutumia miaka isiyo pungua mitatu kurudisha fedha zao walizo wahonga wajumbe na wananchi na kutumia kipindi cha miaka miwili kujiandaa na uchaguzi mwingine pamoja na kujifanya wanawajali wananchi kwa kuliwalisha nyama na vinywaji na kuanzisha miradi mbalimbali ambayo wanaitumia tena kuombea kura wakidai wakiongezwa mitano tena watamalizia miradi hiyo na kufanya zaidi ya hapo.

Hali hii imefanya jamii iamini kuwa siasa ni uongo na mchezo mchafu na wagombea kutoa Rushwa ni sehemu ya siasa na ni sahihi kwa wanasiasa kutoa Rushwa jambo ambalo siyo sahihi.

Watanzania wanatakiwa kufahamu kuwa Rushwa ni adui wa haki na kutoa au kupokea Rushwa ni makosa na ni kuliuza taifa.

Kuna haja ya watanzania kuwakataa viongozi wanao tokana na Rushwa lakini kama wataendelea kukubali viongozi wa aina hiyo ni dhahiri kuwa wataendelea kuvuna wanacho kipanda.