Recent Comments

DIWANI HAFIDH AMWAKILISHA MBUNGE UZINDUZI WA ALBAM KWAYA YA MT. FRANSISCO WA ASIZI.

By Simamia Ngara Sep 22, 2024
Exif_JPEG_420

NA,ANKO G

Diwani wa Kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera amemwakilisha Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndaisaba George Ruhoro kwenye uzinduzi wa Albam ya Tumezitafakari Fadhili Zako ya kwaya ya Mtakatifu Fransisco wa Asizi kigango cha cha Kabanga Kastam kanisa la Mtakatifu Yasinta.

Aidha katika uwakilishi wa Diwani huyo amekabidhi kiasi cha Tsh Milioni moja fedha ambayo ni mchango wa Mbunge kwenye Albam hiyo.

Hata hivyo Albam hiyo ina nyimbo Mbili ambazo ni Wimbo wa Nitakuimbia Eee Mungu wangu na wapili ukiwa ni Tumezitafakari Fadhili Zako ambao ni wimbo unao beba jina la Albam hiyo.

Vilevile Diwani huyo amechangia kiasi cha Tsh Elfu hamsini ambayo ni sehemu ya mchango wake kwa nafasi yake ya udiwani wa Kata ya Kabanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *