CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema kitasimamisha wagombea ubunge 219 kati ya majimbo yaliyopo 265 nchi nzima na kukifanya kuwa cha pili kwa kuwa na wagombea wengi baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimesimamisha wagombea nchi nzima.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema chama hicho kimesimamisha wagombea 44 Zanzibar na 175 Tanzania Bara.
âHii inafanya chama chetu kuwa ni chama cha pili kuwa na idadi kubwa ya wagombea ubunge baada ya CCM ambao wamesimamisha wagombea nchi nzima. Hata hivyo, kati ya wagombea wetu hao, asilimia 25 ni wanawake,â alisema Zitto.
Zitto alisema ACT Wazalendo ni chama ambacho pia kinasimamia maslahi ya vijana kwa sababu ni chama ambacho kimesimamisha wagombea vijana zaidi akitolea mfano kwamba kuna mgombea ubunge kijana kuliko wote ambaye ana umri wa miaka 21.
Alisema chama hicho kinaendelea na semina ya siku mbili kwa ajili ya wagombea wake ili wawe na ujumbe unaofanana wakati wa kampeni urais, wabunge na madiwani na sio kuiimba tu sera ya chama
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments