MSHAURI Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo amesema wananchi hawachagui rais ili awe ofisa miradi, meneja au kufanya kazi za uhandisi kwa sababu wataalamu wa fani hizo wapo isipokuwa anayechaguliwa ni kiongozi mkuu wa nchi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam jana, Profesa Kitila alisema kazi za rais ni nne ambazo ni fikra kwa kuwa ndiye anayestahili kutoa dira ya nchi hivyo anatakiwa kuwa mwenye uwezo wa kufikiri sawasawa.
âKila mnayemsikiliza lazima mumpime kwa uwezo wake na si kwa kumsikia, akisema kwamba ataleta maji au kujenga mitaro kiongozi huyo mkataeni na mwambieni. Sikuhitaji kwa kuwa wataalamu hao wapo na kama ukimuuliza atafanya akakujibu anasubiri ilani ya chama mkataeni kwa kuwa hana fikra za kuongoza nchi,â alisema.
Alitaja kazi nyingine ya rais kuwa ni mlinzi Mkuu wa Tunu za Taifa za msingi kwa kuwa mlinzi wa umoja wa taifa na anatakiwa ajiepushe na tabia za udini na ukanda kwa kuwa ndiye mlinzi wa usawa; kulinda haki za walio wengi ambao ni masikini na asikubali kuwa mateka wa matajiri.
Tunu nyingine anayotakiwa kuilinda ni muungano ambao umelindwa kwa miaka 50, hivyo anatakiwa awe anaujua na asiwe na fikra za kuuchezea awe na uadilifu na mapambano dhidi ya ufisadi.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments