KIONGOZI wa Chama Cha ACT-Wazelendo, Zitto Kabwe, amesema ni vigumu Watanzania kupata mabadiliko kwa viongozi walewale waliowahi kushiriki kuinyonya wakiwa mawaziri wakuu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema Tanzania inapoteza Sh bilioni 900 kwa kila mwaka kwa wafanyabiashara wakubwa wachache wanaotumia ulaghai kukwepa kodi.
Zitto alikuwa akuzungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi ya chama hicho uliofanyika kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala, Dar es Salaam jana.
Alidai siyo CCM wala Ukawa wanaoweza kuzungumzia jambo hilo kwa sababu wanafadhiliwa kwenye kampeni zao na matajiri hao.
âChama pekee kitakachowashukia wakwepa kodi wote ni ACT Wazalendo ambacho kitasaidia kuokoa Sh bilioni 900 ambazo zitaingizwa kwenye sekta ya elimu na afya kwa kutumia mifuko ya jamii,â alisema.
Zitto alisema chama cha ACT-Wazalendo kitasimamia ufisadi wa aina yoyote kwa kuhakikisha kinasimamia na kuendeleza uadilifu kwa kuwataka viongozi wake wanaotaka kuwania madaraka watangaze mali zao kabla ya kuingia madarakani.
Alisema ingawa kila chama kimekuwa kikijinadi kwamba kitapambana na rushwa kwa kutumia miiko ya uongozi, vyama vingine vinaeleza namna ya kuiondoa rushwa huku vikishindwa kueleza namna vitakavyopambana.
âHiyo imechangiwa na nchi hii kuwa na mawaziri wakuu wanaofikia 10 tangu kuasisiwa kwake ambako watatu wamekwisha kufariki dunia.
Wanne waliohai wanaisaidia CCM na wawili wanakiunga mkono Ukawa wakihubiri mabadiliko. Swali ni je, unawezaje kuhubiri mabadiliko kwa mawaziri wakuu waliokuwa kwenye serikali iliyowanyanyasa wananchi wanyonge?â alihoji Zitto na kuongeza:
âTumesikia mmoja wa wagombea akisema watarejesha shirika la ndege hivi tujiulize mwaka 1996 -2002 wakati linauzwa shirika hilo Waziri Mkuu alikuwa nani? Watu wakajibu (Lowassa)â¦hatuwezi kutumia watu walewale kuleta mabadiliko kwa watu waliotuletea matatizo.
âMgombea wa CCM anasema ataleta mahakama maalum ya kushtaki mafisadi⦠wakati tukiwa kwenye bunge la katiba tulitaka Takukuru ipewe meno mgombea wa CCM alikataa leo ameona kuna nini cha muhimu. Hivyo tunatakiwa kutambua kwamba chama chenye kufanya mabadiliko ni ACT chini ya mgombea wetu Anna,â alisema Zitto.
Kiongozi huyo wa ACT alibeza ahadi iliyotolewa na CCM kutoa Sh milioni 50 kwa kila kijiji. Alisema kwa vijiji vyote Tanzania nzima itagharimu Sh bilioni 600 ambazo ni sawa na bajeti ya wizara nzima ya kilimo, bila ya kueleza mahali watakapozipata.
Mgombea Urais
Mgombea urais wa chama hicho, Anna Mghwira alisema iwapo atapata nafasi hiyo atahakikisha anamteua kiongozi mkuu wa chama hicho na kuwa waziri wake mkuu waweze kushirikiana katika kuleta mabadiliko ya fikra na sera.
Alisema akichaguliwa kuwa rais wa tano atahakikisha analinda utu, uzalendo na uadilifu ambao uliasisiwa na Mwalimu Nyerere lakini sasa umeporomoka kwa kiasi kikubwa.
Mgombea huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema akipewa nafasi atatengeneza serikali itakayolinda Muungano, itakayojumuisha mashirika ya dini na asasi za raia kwa sababu anaamini taifa halina dini.
Alisema na serikali yake itaapishwa Dodoma kama alivyofikiri Mwalimu Nyerere kwa kuwa mkoa huo ndiyo makao makuu ya Serikali.
Mabango yaliyokuwapo
Wakati huo huo, mkutano huo ulipambwa na mabango mbalimbali baadhi yakisomeka: âKuzikwa na wengi siyo kwenda peponiâ, âACT chama kitakachongâoa weziâ, âAnna ni mpambanaji wa kweliâ, âACT ndicho chama mbadala wa CCMâ, âACT chama kinachojali akina mamaâ.
âHakuna kama ACTâ, âMwisho wa CCM Oktoba 25â, âWazalendo wa kweli ACTâ, âZitto mbabe waoâ, âhatulei mafisadiâ, âwaadilifu wapo ACTâ, âCCM majizi hayana uzalendoâ, âACT mkombozi wa taifa letuâ, âWatanzania wanataka fikra pevuâ na âwazendo wasiotumia fedhaâ.
Recent Comments