Na Bakari Kimwanga
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kama kungekuwa na mashindao ya ilani bora ya uchaguzi, chama chake kingeongoza kwani kina ilani nzuri kuliko vyama vingine.
Alisema vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), havina ilani inayoweza kutatua matatizo ya Watanzani hivyo ni vyema wananchi wasihadaike nao.
Ukawa inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, walizindua kampeni na ilani yao juzi jijini Dar es Salaam na kuweka vipaumbele vyao ikiwamo kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya chekechea mpaka chuo kikuu na kila mwananchi kupata tiba bora na nafuu.
Jana Dk. Magufuli akihutubia wananchi kwenye mikutano iliyofanyika katika wilaya za Ludewa na Songea, alisema ilani ni mkataba kati ya wananchi na chama kinachoomba ridhaa lakini hilo limekuwa tofauti kwa vyama vya Ukawa.
âSijui kuna vyama vitano vimeungana na kuwa na ilani moja ya uchaguzi, hapo hakuna kitu, chama chenye mgombea ndicho kinakuwa na ilani.
âIlani ni mkataba kati ya wananchi na chama kinachoomba ridhaa, sasa Ukawa ni muungano wa vyama, ilitakiwa kila chama kiwe na ilani yake, Ukawa hawana ilani ila CCM ndiyo imejipanga kuomba ridhaa na ina ilani bora na yenye kutekelezeka kwa uhakika,â alisema Dk. Magufuli.
Kutokana na hali hiyo, alisema anaomba urais si kwa ajili ya kufanya majaribio ila anataka kuwatumikia Watanzania kwa vitendo.
âNinapenda kuwaambia leo nipo hapa Ludewa lakini mbunge wenu ni mbunge mkweli na mfuatiliaji wa mambo.
âBaada ya uchaguzi tunaanza kuitengeneza hii barabara kutoka Njombe hadi Ludewa ili kuchochea na kuimarisha uchumi, Filikunjombe pamoja na wananchi ni lazima niwape zawadi ya lami.
âLudewa ina mradi mkubwa wa makaa ya mawe, ni lazima tufungue njia⦠ninajua hapa kuna tatizo la maji nitashughulikia kwa wakati,â alisema Dk. Magufuli.
Filikunjombe na kilio
Awali akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Mlangali, Mbunge mteule wa Ludewa, Deo Filikunjombe, alisema anatambua utendaji kazi wa Dk. Magufuli.
Alisema pamoja na hali hiyo, lakini bado kuna changamoto kadhaa ikiwemo tatizo la maji safi na salama katika kata hiyo
Recent Comments