MGOMBEA ubunge wa Kahama mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), James Lembeli, amewataka watanzania kupuuza propaganda inayoenezwa kuwa mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, ni msukuma ili kuwarubuni watu wa Kanda ya Ziwa wampigie kura.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu ujao za Ukawa katika Wilaya ya Shinyanga uliofanyika jana katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga, Lembeli alisema siyo kweli kwamba Magufuli yuko pamoja na watu wa Kanda ya Ziwa.
Lembeli alisema hakubaliani na propaganda inayoenezwa na wafuasi wa CCM kuwa kwa vile Magufuli ni msukuma hivyo wasukuma wamuunge mkono kwenye mbio zake za kuutaka urais.
âSikubali kabisa, mimi nilikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge iliyochunguza dhambi na shida waliyopatiwa wafugaji wakiwamo wasukuma ambao waliuawa, waliteswa na kuibiwa mali zao lakini Magufuli anayedaiwa kuwa ni msukuma hakufungua mdomo wake kutetea ndugu zake,hatukubali,â alisema Lembeli.
Lembeli alisema a kitendo hicho cha kukaa kimya dhidi ya vitendo viovu walivyotendewa wafugaji hao, inadhihirisha kuwa hayuko pamoja na wasukuma hivyo asionewe huruma bali watanzania wamchague Edward Lowassa ambaye ni jasiri na msema kweli.
Mgombea ubunge wa Chadema katika jimbo la Shinyanga mjini, Patrobas Katambi, aliwataka wakazi wa Shinyanga kushikamana na kuepuka vitendo vya usaliti na kuhakikisha kuwa wanawapa kura wagombea wa Ukawa badala ya kuishia kushangilia katika mikutano ya hadhara.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments