MGOMBEA Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Didas Massaburi amekiri kuwapongeza vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walioandamana kuunga mkono hotuba ya aliyekuwa Katibu Mkuu wao, Dk Willibrod Slaa na kujiunga na CCM, akisema anakubaliana na hoja zilizotolewa.
Pamoja na kukiri hilo, Dk Massaburi amesema ataendelea kuwapokea, kuzungumza, kuwaunga mkono na kuwapongeza, vijana wote wa Chadema na CUF watakaokubaliana na hoja za Dk Slaa na kuvihama vyama vyao na kujiunga na CCM kwa vile kujiunga kwao ni mtaji kwa chama chake.
Aliyasema hayo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana kutoa ufafanuzi juu ya shutuma kwamba alipanga na kuratibu maandamano ya vijana wa Chadema walioandamana juzi hadi Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni na kurejesha kadi, lakini baadaye wakakumbana na kipigo cha wanaChadema wenzao na polisi.
âKuhusu kuwapongeza ni kweli kabisa niliwaita na kuwapongeza tena hapa hapa ndani (Ofisi ya CCM Tawi la Manzese). Nilifanya hivyo kwa sababu mimi binafsi nakubaliana kabisa na hoja za Dk Slaa.
Naweza nikawa natofautiana naye kwa masuala mengine kama ya kiitikadi na kimsimamo, lakini hoja alizozitoa juzi nazikubali asilimia mia moja. âNdio maana sikusita wakati Diwani wa Kimara kupitia Chadema (bila kumtaja jina) alipokuja kwangu na kuniambia wapo vijana wanaunga mkono hoja za Dk Slaa na wapo tayari kufanya maandamano ya amani kwenda kurejesha kadi zao na kujiunga CCM.
Hata angekuwa ni Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa Chadema Taifa), anakubaliana na Dk Slaa ningemuunga mkono,â alisema Dk Massaburi. Alisema kutokana na hilo, haoni ubaya kwa yeye kuwaita vijana hao na kuwapongeza baada ya kurejesha kadi za Chadema na kupewa za CCM na kuongeza kuwa ataendelea kuwapokea vijana wengi zaidi watakaorejesha kadi za Chadema na CUF na kujiunga na CCM, katika ofisi hiyo ya Jimbo iliyopo Manzese.
âKinachotakiwa hapa ni kwa Ukawa kujitokeza na kujibu hoja za Dk Slaa sio kungâangâania hoja ya Dk Massaburi tu. Wajibu hoja ni vipi watu waliokuwa wakiwaita wachafu na mafisadi, leo wamekuwa wazuri na watakatifu walipotoka CCM na kuhamia kwao,â alisema Meya huyo wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam.
âLeo kama mnavyoona bado wengine wanaendelea kurejesha kadi za Chadema na CUF, sasa nimewaelekeza walete hapa. Hiki ndio kitakuwa kituo cha kupokelea kadi za Ukawa na kupewa za CCM kwa Jimbo la Ubungo.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wengine 50 wa Chadema na CUF waliorejesha kadi zao na kuzikabidhi kwa Dk Massaburi katika mkutano huo na wanahabari jana, mwanachama wa CUF, Mbwana Abdallah alisema hawezi kubakia katika vyama visivyo na msimamo.
Recent Comments