WANACHAMA WA CHADEMA ZAIDI YA 500 LUDEWA WAHAMIA ACT WAZALENDO ,WACHUKIZWA NA LOWASA KUPOKELEWA CHADEMA NA KUKATWA KWA MSHINDI WA KURA ZA MAONI
Baadhi ya wafuasi wa chama wa Chadema wamehamia chamia chama cha ACT – Wazalendo baada ya kutolidhishwa na walichokiita ubinafisi, ukabila na kupendekeza upenzi wa pesa kuliko utumishi na uzalendo kwa nchi yao. Wamedai kutolidhishwa na maamuzi mengi yaliyofanywa na wakubwa wa chama cha chadema na kutowekea maanani katika kusikiliza na kutii maoni ya wananchi. Baadhi ya yale waliotaja na kupelekea kusikitishwa na chama chao cha zamani ni pamoja na pamoja na kukubali Lowassa kugombea Urais, wananchama mpya ambaye alikimbia chama chake cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuona kanyimwa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM kama mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Chini ya siku tano baada ya kujiunga na chama cha chadema, Lowassa aliteuliwa kuwa mgombea wa urais huku mwanzilishi wa chama hicho, Daktari Willibrod Slaa akilazimika kuzihuzuru kwenye uongozi wa chama hicho. Hapo awali, Dk. Slaa amezihuzuru kwa kuwa hakutaka kuongozwa na Lowassa ambaye chama cha Chadema kilimuita fisadi. Matendo ya ufisadi ndio yamepekea nchi ya Tanzania kuwa masikini ulimwenguni. Lowassa ameshindwa kuleta maendeleo katika miaka zaidi ya 25 aliyokua serikalini, iweje leo mtu mwenye akili zake akubali uongo anaotangazania wananchi eti ataokoa nchi na kuleta maendeleo ya kiuchumi hasa ukizingatia muhura mmoja wa urais ni miaka mitano tu. Dk. Slaa aliuliza swali la kutafakari, unaanzaje na fisadi halafu unadai nia yako nikumaliza ufisadi huku unatumia kiungo kile kile kilichokuwa kinatokomoza uchumi wa nchi yetu kutokana na matendo yake machafu?
Lowassa alitumwa serikalini akawakilishe wananchi waliomchagua. Yeye miaka yote aliokuwa madarakani ameitumia kujitajirisha yeye na familia yake. Anadai ataleta umeme vijijini huku hata jimbo lake alilowakilisha Bungeni miaka yote hiyo halina umeme jimbo lote.
Profesa aliobobea kwenye fani ya siasa, profesa Mungwaida ameliambia gazeti hili eti Lowassa anadai alijenga shule za kata huku mpango mzima uliandaliwa katika kipindi cha rais Mkapa. Yeye amefanya kusimamia huo ujenzi chini ya uongozi wa rais Kikwete.
Kati ya wananchi waliongea na mwandishi wetu wameambia gazeti la simamia ya kuwa Chadema sasa ni kama jalala ambapo makapi yanahifadhiwa na hata kupewa nafasi ya kuwania baada ya wanachama wazalendo waliokuwa na chama kwa muda mrefu. Wamedai Chama Cha Chadema imekua ni kama jalala ambapo wengi wanakimbilia wanashindwa kutimiza matakwa yao kwenye chama cha Mapindizi.
Zifatazo ni baadhi ya picha zilizofikia gazeti la Simamia.
Wanachama wa Chadema wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe wakiandamana kupinga maamuzi ya chama hicho kukata jina la mshindi wa kura za maoni na kumteua aliyeshindwa ,mbali ya kuandamana pia wanachama hao zaidi ya 500 walikihama chama hicho na kujiunga na ACT Wazalendo.
Wanachadema wakiwa nje ya ofisi ya chama wilaya walikokwenda kurudisha kadi kabla ya kuhamia ACT wazalendo.
Wanachadema wakiwa nje ya ofisi ya ACT Wazalendo ambako walifika kuomba kujiunga huko.
Wanachadema wakirudisha kadi za chamna hicho na kujiunga na ACT wazalendo.
New Picture (11)
Kadi zikiwa zimekusanywa kwa kuchomwa moto.
Hivi ndivyo kadi zinavyoteketezwa kwa moto baada ya wana Chadema kujiengua na chama hicho na kujiunga na ACT wazalendo.
Hasira za kukatwa kwa mshindi wa kura za maoni Ludewa.
Wanachama wa Chadema waliohamia ACT wazalendo wakiwa na mabango ya kukituhumu chama hicho kwa kukiuka Demokrasia.
Recent Comments