Lowassa: Msikose usingizi
*Amwaga ahadi, asema hakuna kura itakayoibwa
*Mnyika amfananisha Dk. Slaa na Samsoni, Delila
NORA DAMIAN NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM
MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ameisimamisha tena Dar es Salaam kwa saa kadhaa huku akiwataka Watanzania kutokosa usingizi kwani hakuna kura itakayoibwa.
Lowassa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti alipokuwa kwenye mikutano ya kampeni Wilaya ya Kinondoni katika majimbo ya Kawe na Kibamba.
Akiwa katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi, Bunju A kwenye Jimbo la Kawe, alisema watu wasikose usingizi bali wasubiri Oktoba 25 ifike.
Licha ya kwamba Lowassa alifika Bunju saa saa 9:25 alasiri, viwanja hivyo vilianza kufurika watu kuanzia asubuhi kwani mkutano ulitarajiwa kuanza saa 5:00 asubuhi.
Hali ilikuwa hivyohivyo kwenye Jimbo la Kibamba ambako licha ya kiongozi huyo kufika katika eneo hilo saa 11:30 jioni, watu walianza kufurika asubuhi, hali iliyofanya barabara ya Morogoro kupitika kwa shida.
MSIKOSE USINGIZI
Akizungumza katika Mkutano wa Kawe, Lowassa alisema shaka dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), iliyopo sasa inatokana na jeuri ya wapinzani wao.
âKuna maneno mengi yanasemwa kuhusu NEC⦠nawahakikishieni hawataiba ngâo, tuko imara, tutalinda kura zetu hadi zitakapohesabiwa.
âNEC na CCM hamtaweza kuiba kura zetu, Watanzania tukatae kuibiwa kura na kulaghaiwa,â alisema Lowassa.
Aidha Lowassa alisema kuna watu wa ofisini wanataka mageuzi, lakini wanatishwa, na wengine ni wafanyabiashara wanaotaka kutusaidia.
âHao wanaowatisha walie tu, hawawezi kumshughulikia mtu yeyote,â alisema.
Alisema atabadilisha mfumo wa utendaji kazi wa Serikali kutoka ulivyo sasa na kuwa wa kasi. âItakuwa ni spidi 120â, alisema.
Aliendelea kusema: âZimebaki siku 48, tukatae msongamano wa magari Dar es Salaam, adha na tabu katika hospitali na vituo vyetu vya afya, michango ya shule za sekondari na msingi, tatizo la maji na ajira.
âFanyeni uamuzi mgumu tuibadilishe wizara ya elimu, tuwe na kilimo cha kisasa na kuanzisha viwanda kwa ajili ya vijana wetu nchini,â alisema.
SUMAYE
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye alipanda jukwaani saa 9:55 alasiri na kuonya kuwa kama CCM haitakubali kushindwa inaweza kusababisha machafuko.
âNchi hii iko kwenye mfumo wa vyama vingi na ili viwe na maana lazima kila chama kiwe tayari kushindwa kama hakijafanya vizuri, lakini CCM hakitaki, hali hii ni hatari sana.
âLibya, Misri na Tunisia zimefika zilipofikia kwa sababu waliokuwa kwenye madaraka walikuwa hawataki kuachia na kukandamiza watu. CCM isipokubali mabadiliko itakuwa inataka yale ya Gadafi,â alisema Sumaye.
Alifananisha matusi yanayotolewa na wapinzani wao dhidi yake na Lowassa kuwa ni sawa na kumpiga teke chura.
âWanatengeneza timu za kututukana, lakini nawaambia hapo ni sawa na kumpiga teke chura. Lowassa alitoka serikalini miaka minane iliyopita na tume ya Bunge ilisema hakukuwa na jambo lililomgusa moja kwa mojaâ¦alijitosa ili kumuokoa rais na Serikali yake,â alisema.
Waziri Mkuu huyo pia aliibeza hoja ya mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli kuwa hataweza kupambana na rushwa kwa sababu tayari ameonyesha udhahifu katika wadhifa aliokuwa nao wa Waziri wa Ujenzi.
âUtabadilishaje Tanzania wakati leo hii wewe ni waziri, lakini kwenye mizani kumejaa rushwa?
âAtaitoa wapi nguvu ya kupambana na rushwa, ndani ya CCM huwezi kufanya kitu chochote,â alisema.
Sumaye pia alisema kitendo cha kutoweka jina la chama katika mabango ya mgombea urais wa CCM kinaonyesha kuwa ndani ya chama hicho hali ni mbaya.
âMabango yanasema âChagua Magufuliâ hayasemi âChagua CCMâ, kama anajua CCM haimpeleki kokote si angekuja Ukawa?
âMimi niko Ukawa, lakini sigombei urais, kazi yangu ni kuwakomboa wananchi,â alisema Sumaye na kuongeza kuwa âCCM ni shidaâ.
MBOWE
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alitamba kuwa wananchi wote wako tayari kufanya mabadiliko.
âTumekwenda Iringa, Njombe, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora na leo (jana) tuko Dar es Salaam, nchi imeshalegea na iko tayari kwa sababu ya Lowassa,â alisema Mbowe.
Huku akiwaelekeza wananchi kuzungusha mikono kama ishara ya kufanya mabadiliko, Mbowe alionya kuwa kama machafuko, basi yataletwa na NEC kutokana na kitendo chao cha kujaribu kuibeba CCM.
âSasa hivi CCM haibebeki hata ukileta mbeleko, wanawatumia baadhi ya watu kumchafua Lowassa, Sumaye na wote walioondoka CCMâ¦wapuuzeni watu wamefika bei,â alisema.
MDEE
Mgombea ubunge katika Jimbo la Kawe, Halima Mdee, aliomba idhini ya viongozi wa chama hicho kufanya maandamano ya kuishinikiza NEC kuacha kufanya hujuma.
âTuna mashaka na zoezi linaloendelea la uhakiki, kuna watu wanaandikisha vitambulisho vya vijana na kina mama, CCM na NEC wanataka kufanya uhuni.
âTunaomba kauli yenu kama ikibidi tuandamane hadi NEC tukakinukishe, tutafanya hivyo,â alisema Mdee.
Kwa mujibu wa Mdee,katika jimbo hilo wamefanikiwa kutatua migogoro ya ardhi katika eneo la Chasimba na Nakerekwa, lakini bado kuna mgogoro katika eneo la Boko kwa Sonji ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 20 na katika eneo la Magereji lenye vijana zaidi ya 4,000.
âMtaji wa vijana hawa wa gereji ni zaidi ya Sh bilioni tano na wamekaa hapa tangu mwaka 2007, lakini leo hii wanaambiwa waondoke,â alisema.
MWALIMU
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu, alisema CCM wameishiwa sera na sasa wanafanya matamasha ya burudani.
âMagufuli anazunguka nchi nzima kufanya matamasha ya burudani badala ya kunadi ilani ya chama chakeâ¦ukiingia muachie wizara ya utamaduni,â alisema Mwalimu.
KUWASILI UWANJANI
Maelfu ya wananchi walianza kuwasili viwanjani hapo saa 3 asubuhi na ilipofika saa 7 mchana uwanja ulikuwa umejaa.
Baadhi ya watu walilazimika kupanda juu ya miti na wengine kupanda juu ya mapaa ya Shule ya Msingi Bunju A ili waweze kushuhudia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano huo.
Waendesha bodaboda walikuwa ni kivutio pekee katika mkutano huo kwani wengine walionekana kuendesha pikipiki kwa mbwembwe kubwa huku wakipaa juu na wengine walikuwa wakizunguka uwanja huo mara kwa mara.
Baadhi ya watu walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kama vile âDk. Slaa kiapo cha kanisa kimekuponza uchizi unakunyemeleaâ na âulipo tupoâ.
JIMBO LA KIBAMBA
Katika mkutano uliofanyika Jimbo la Kibamba kwenye Uwanja wa Mbezi Mwisho, Lowassa alisema hana muda wa kubishana na wanachama wa CCM wanaomtukana majukwaani, na kwamba watakutana katika sanduku la kura.
âMahaba yananifanya nijiamini, ndiyo maana ndugu zangu wanahangaika nikiwa na nguvu ya umma kama hii, nawaambia tukutane kwenye sanduku la kura,â alisema.
Lowassa alisema endapo watu wanataka mabadiliko katika maeneo mbalimbali ikiwamo elimu, wanapaswa kuandaa shahada zao na kuwapigia kura wagombea wa Ukawa Oktoba 25.
Naye Sumaye alisema katika uchaguzi wa mwaka huu CCM lazima itoke madarakani hata kama haitaki.
âCCM hakitaki kutoka madarakani hata kama watu hawakitaki, wanatumia hila zote, tunasema safari hii mtatoka tu ,mnahangaika kuchafua viongozi, mnanihangaika hadi mimi ambaye sigombei,â alisema Sumaye.
Alisema kitendo cha wanachama wa CCM kujipanga na kumtukana hakisaidii badala yake kinamwongezea nguvu ya kupigania maendeleo.
Sumaye alisema alikihama chama hicho kwakuwa kimeshapoteza matumaini ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
MNYIKA
Mgombea ubunge Jimbo la Kibamba, John Mnyika, alimfanisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa na Samson wa kwenye Biblia aliyedanganywa na Delila.
âMnamfahamu Samsoni wetu? Alisema tumemchukua mtu chooni tukamwingiza chumbani, amesahau kwamba yeye katoka chumbani ameenda chooni, msiendelee kumsikiliza Samsoni, mpuuzeni hana jipya.
âMzee wetu kadanganywa ameenda chooni kuwaunga mkono CCM,â alisema Mnyika.
Katika hatua nyingine, alimtaka Lowassa akiingia madarakani kuangalia tatizo la maji ambalo ndilo kubwa ndani ya jimbo la Kibamba.
Naye Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe, aliituhumu CCM kuwa inatumia Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) kukwepa kodi ya mafuta ili ikusanye Sh bilioni 50 za kununua shahada za kupigia kura.
âKuna mkakati wa kuitumia TRA kuingiza mafuta ambayo hayatalipiwa kodi ili wapate Sh bilioni 50 kwa ajili ya kuwasaidia kununua shahada za kupiga kura. Tunawaambia tumewabaini na waache mara moja huo mchezo, tunataka watukabidhi nchi ikiwa na hazina ili tuweze kuleta mabadiliko ya kweli,â alisema Mbowe.
Alisema anao ushahidi ju ya hilo na kuongeza kuwa CCM inaweweseka mwaka huu.
Recent Comments