MGOMBEA ubunge jimbo la Tandahimba, mkoani Mtwara anayewakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Katani Ahmad Katani ameidhinishwa kuendelea kuwa mgombea. Anaandika Hamisi Mguta ⦠(endelea).
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesikiliza rufaa sita za ubunge na udiwani, na kuzitolea maamuzi ikiwemo iliyomhusu Katani ambaye anagombea kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF).
Katani alikatiwa rufaa na mgombea jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Likumbo Shaibu Salim.
Wagombea wengine ambao rufaa zao zimeamuliwa na kuidhinishwa kugombea, ni pamoja na Profesa Jumanne Maghembe, anayegombea jimbo la Mwanga (CCM) ambaye ni Waziri wa Maji katika serikali inayomaliza muda. Alikatiwa rufaa na Henry Kilewo (Chadema).
Wengine ni Dk. Abdallah Kigoda anayetetea kiti jimbo la Handeni Mjini, mkoani Tanga ambaye alikatiwa rufaa na Daudi Killo (Chadema).
Naye Daniel Nsanzugwanko ambaye anagombea ubunge jimbo la Kasulu Mjini (CCM), ameidhinishwa na Tume kugombea kwa kushinda rufaa iliyokatwa na Bunyago Gideon wa NCCR-Mageuzi.
Wengine ni Youngsaviour Msuya anayegombea ubunge Mwanga (NCCR-Mageuzi), ambaye alikatiwa rufaa na Henry Kilewo wa Chadema na Dismas Luhwago (Chadema) anagombea jimbo la Wangingâombe. Alikatiwa rufaa na Gerson Lwenge wa CCM.
Maamuzi hayo yametolewa baada ya kikao cha Tume kujadili na kufikia uamuzi wa kukubali na kukataa rufaa hizo.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpigakura wa Tume, Giveness Aswile amesema rufaa sita za wabunge kati ya 13 zilizokuwa hazijafanyiwa uamuzi kutokana na kukamilika kwa vielelezo vyake.
Katika rufaa hizo, Tume imezikataa sababu za rufaa zote na kukubaliana na maamuzi yaliyotolewa na wasimamizi wa uchaguzi wa maeneo yao.
Aswile amesema tayari rufaa 70 za madiwani kati ya rufaa 118 zilizokuwa hazijaamuliwa kutokana na vielelezo vyake kutokamilika na uwamuzi wa Tume utafuatwa kama ulivyopangwa.
Amesema kati ya rufaa zilizoamuliwa, rufaa 14 zilikubaliwa na Tume, ikiwa na maana kuwa maamuzi hayo yamewarudisha wagombea waliokuwa wameenguliwa kugombea.
âTume imetengua maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi na kuwarejesha wagombea katika kinyangâanyiro cha udiwani ndani ya kata zao,â amesema Aswile.
Aidha, Tume imekataa sababu zilizotolewa kwa rufaa 58 na kuridhia maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi âwagombea watafuata maamuzi yaliyotolea na wasimamizi wa majimbo na Kata husika.â
Recent Comments