ALIYEKUWA Waziri Mkuu wa awamu ya tatu kwa miaka kumi mfululizo, Frederick Sumaye aliyejiunga Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), amesema mwaka huu ni mwaka wa kuizika serikali ya CCM na kuwashughulikia wezi wa mali za umma. Anaandika Dany Tibason, Bahi ⦠(endelea).
Mbali na kutangaza kuizika CCM amewataka watanzania kupuuza vitisho ambavyo vinatolewa na wana-CCM kwa madai kwamba upinzani ukichukua nchi kutatokea machafuko.
Sumaye alitoa kauli hiyo wilayani Bahi katika mkutano wa kuzindua kampeni ya ubunge uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Bahi Sokoni wilaya ya Bahi, Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, pia alimnadi Mgombea ubunge, Mathius Lyamunda (Chadema).
Sumaye amesema kutokana na mfumo mbovu wa serikali ya CCM ndiyo maana kuna mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na vyakula.
âSerikali imekuwa ikilalamika eti kuna mawaziri mizigo mawaziri mizigo wanateuliwa na nani? Si kwa sababu ya kuteuliwa kishemeji shemeji kwa sasa serikali ya CCM ni sawa na shetani siyo CCM ya zamani,â amesema Sumaye.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge wa jimbo la Bahi, Lyamunda amemuomba Mgombea Urais, Lowassa kama akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania kuhakikisha madini ya Uranium hayatoki wilayani Bahi.
Lyamunda amemtaka Lowassa mara atakapochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha madini ya Uranium hayatoki katika wilaya hiyo.
âNdugu Rais watu wananchi wa jimbo la Bahi kilio chao kikubwa wanataka usitishe mpango wa madini ya Uranium kutoka katika Jimbo hili,ââamesema Lyamunda huku akishangiliwa.
Aidha Lyamunda pia amesema kilio kingine cha wakazi wa wilaya hiyo ni ukosefu wa maji kwa kuhakikisha yanapatikana ili kuondoa tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda.
Amesema pia aliitaka serikali hiyo kusimamia suala la mradi Farkwa kwani utawafanya washindwe kufanya shughuli zao muhimu kama za ufugaji pamoja na umwagiliaji.
Lyamunda amesema suala la wafugaji kulipishwa michango mingi nalo limekuwa ni tatizo hivyo kama akipata nafasi aliangalie kwa umakini ili kuisaidia jamii ya Bahi kujikwamua kihuchumi na kuondokana na umaskini.
Kuhusu suhala la tatizo la maji, Lyamunda amesema: âMheshimiwa rais pia kuna hili suala la Mto Bubu hasa huu mradi wa Farkwa, maji kwenda Dodoma na asilima 10 kuja huku kwetu, hapa tunategemea kilimo na ufugaji, tunakuomba suala hilo lipatiwe ufumbuzi ili wananchi waweze kutumia maji ya uhakika katika shughuli zao za maendeleo,â amesema Lyamunda.
âMaji ni jambo muhimu kwa maendeleo ya wananchi hivyo, linatakiwa kupatiwa ufumbuzi mara tu uingiapo Ikulu ili kuwafanya wananchi kupata maji safi na salama,â amesema Lyamunda.
Naye mgombea Urais kupitia UKAWA, Edward Lowassa aliwahakikishia wakazi wa jimbo hilo kama wakimpa nafasi kero zote walizonazo atahakikisha anazitatua.
Amesema ili kazi iweze kuwa nzuri na ya uhakika anawaomba wananchi wa Bahi na mikoa mbalimbali nchini kuhakikisha wanamchagulia wabunge wengi makini ambao wanatokana na UKAWA ili kuirahisisha kazi.
Mbali na hilo Lowasa amesema amefurahishwa sana na kitendo cha wananchi wa Bahi kumfanya kuwa chifu wao na kuahidi kuwa atawatumikia wananchi kwa malengo mapana ya kimaendeleo.
Recent Comments