MWENYEKITI wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amemvaa mgombea wa urais kupitia Chadema, Edward Lowassa na wengine waliohamia Ukawa akisema wanashukuru chama kimetua mzigo.
Msukuma, ambaye anaaminika kuwa swahiba wa Lowassa wakati wa mchakato wa kura ya maoni kwenye CCM, aliuambia mkutano jana kwamba hakuna anayefahamu siri za Lowassa.
âNataka nimwambie ndugu yangu, rafiki yangu Lowassa, huu ni muziki mkubwa,â alisema Msukuma kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea wa urais wa CCM, Dk John Magufuli uliofanyika jana mjini Chato, mkoani Geita.
Msukuma ambaye aliponda waliohama CCM baada ya kura za maoni kwa kutaja majina ya baadhi, akiwalinganisha na bendera inayofuata upepo na kusisitiza kuwa wenye akili hawahami.
âTumeshukuru sana CCM tumetua mizigoâ¦â, alisema Msukuma ambaye ni mgombea ubunge, Jimbo la Geita Vijijini akiwataja Lawrence Masha, Msindai, Mngeja akisema wamehamia Ukawa si kwa mapenzi mema isipokuwa, ni kutokana na kukosa ushindi kwenye kura za maoni.
âTuna hasara gani Masha akihama CCM?â alihoji umati ambao uliitikia kwa kusema hakuna hasara. Msukuma ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa CCM waliohudhuria mkutano wa Lowassa uliofanyika Arusha wakati wa mchakato wa kura za maoni, akisifia mkutano wa jana wa Magufuli, alisema, âToka niwe mwenyekiti sijawahi kuona watu wengi kama hawa.
Hata nilipoteremka Arusha na chopa, haikuwa hivi.â Alieleza kushangazwa na baadhi ya picha zilizooneshwa kuwa ni za mkutano wa Lowassa mjini Chato na kusema mandhari iliyooneshwa, haikuwa ya uwanja huo wa stendi.
âStendi ya Chato haina miembe wala lami,â alisema. Akiendelea kuponda waliohama, alisema, kama Dk Magufuli angekuwa anatoa rushwa, wasingehama. âHakuna hasara na wote waligombea wakashindwa,â alisema na kueleza kumfahamu Mngeja kwa kuwa walikuwa wakikaa kwenye helikopta moja.
âTunaomba wachukue na wengine wenye tabia kama hizo. Wenye akili timamu tutabaki CCM…Mgombea wetu (Magufuli) anatosha. Na hapa ndiyo kwaoâ¦nimetembea na Lowassa gari moja, ndege moja, tunachagua rais na sio bora raisâ¦,â alisema.
Alisisitiza, âKatika Kanda ya Ziwa, hakuna aliye na siri za Lowassa kama mimiâ¦naomba waniweke kwenye mdahalo nitagharimia, niwapige kavu kavu. Watu wanaokwenda kule (Ukawa) zinatangulizwa hela. Nani anachukia hela?.â
Aliendelea kusema, ânajua mengi ya kambi ile nilikwenda kufanya kazi. Hata wale wachungaji waliokwenda Dodoma, ni wachungaji feki walionunuliwa.â Mke wa Magufuli Mke wa Magufuli, Janeth, alishukuru wana Chato kwa kumpa heshima kubwa mbunge wao kwa kipindi chote cha miaka 20 hadi chama kikamteua kuwa mgombea urais.
Wakati akizungumza, zilisikika sauti kutoka kwenye mkutano zikishangilia ârais raisâ. Mke huyo wa mgombea aliomba Oktoba 25 wana Chato wamchague kwa wingi. Aliomba pia wamchague Dk Medard Kalemani kuwa mbunge wa Chato. Ameomba pia wachague madiwani wa CCM wapeperushe bendera vyema.
Recent Comments