MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli amewaaga rasmi wananchi jimboni kwake Chato, mkoani Geita kwa kuwashukuru na kueleza namna alivyofikia uamuzi wa kugombea nafasi hiyo ya juu, huku akisema hata akiwa Rais wa Tanzania, kamwe hatabadilika.
Aidha, ameendelea kusisitiza kuwa, atakuwa Rais wa Watanzania, bila kujali dini, kabila au vyama, hivyo maendeleo ya serikali yake hayatabagua. Akizungumza jana mjini hapa kwenye mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya watu ambao alikiri kuwa ni mkubwa ambao hajawahi kuuona, amewahakikishia kuwa ataiendesha nchi kwa ustaarabu na si kwa udikteta kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidai.
âHata baada ya kuchaguliwa, mimi sitabadilika, nitabaki kuwa mtoto wenu yule yule John Magufuli,â alisema na kuongeza; âNitaiendesha nchi kwa ustaarabu, sitaiendesha nchi kwa udiktetaâ¦pamekuwa na watu wanazungumza, kwa sababu nazungumza ukweli na ukweli utabaki ukweli kweli. Watu wanabaki kutishiana. Nyie wana Chato waelezeni ukweli kwamba nilipokuwa waziri nilikuwa nachunga ngâombe, nilikuwa nakamua maziwa.
Mimi kazi ni kazi.â Magufuli aliwaambia wananchi hao waliompa ubunge kwa miaka 20 mfululizo, kwa kuwaambia kwamba, wanaompiga vita ni mafisadi wanaoogopa jeuri yake ya kusimamia kazi na utendaji. Akizungumzia uamuzi wake wa kugombea urais, alisema alijipima kwenye moyo wake kwa kumtanguliza Mungu. Alisema ameomba nafasi hiyo si kwa majaribio bali anaamini na kujiamini kwamba atakapokuwa rais atasimamia mambo mengi na kuifanya Tanzania mpya.
âNafahamu tumetoka mbali, tumefika mbali na tunaelekea mbali. Niliomba nafasi ya urais si kwa majaribio bali nataka niwatumikie watanzania,â alisema na kusisitiza kwamba anafahamu kwa dhati bila kubagua vyama, makabila, wanataka mabadiliko kwa maana wanataka maendeleo na Tanzania mpya. Ashukuru mapokezi Dk Magufuli aliwashukuru wananchi na kusema, mapokezi ya namna hii hayajawahi kutokea.
Huku akishangiliwa mara kwa mara, aliwashukuru wananchi hao kwa kushirikiana naye kwa raha na shida akiwa mbunge wao kwa miaka 20. Alisema katika kipindi cha miaka 10 mfululizo, wananchi walimpitisha bila kupingwa. âNafahamu tumetoka mbali, tumefika mbali na tunaelekea mbali.
Niliomba nafasi ya urasi si kwa majaribio bali nataka niwatumikie watanzania,â alisema. Aliongeza kuwa, anafahamu kwa dhati bila kubagua vyama, makabila, wanataka mabadiliko kwa maana wanataka maendeleo na Tanzania mpya.
Alisema alijipima kwenye moyo wake kwa kumtanguliza Mungu na anaamini yuko tayari kuwapatia Tanzania mpya. Magufuli ambaye amekuwa akisisitiza suala la amani, alipongeza marais waliotangulia kwa kusimamia amani ya nchi na kuamini kuwa Tanzania ni moja.
Alisema yako mengi yamefanyika katika awamu zote. Lakini yanawezekana, yaliyofanyika yanaweza yasionekane licha ya mengine kuwa kwenye maeneo yao. Alieleza kushangazwa na baadhi ya watu kusema hakuna chochote kilichofanyika.
Alielezea Chato ilivyokuwa na kusema kilikuwa kijiji na nyumba za bati hazikuwa nyingi kama hizi. Alitaja pia barabara za lami hazikuwepo, shule za msingi zilikuwa nne wakati sasa zipo zaidi ya shule 130.
âLakini bado kuna mtu anaweza kusimama akasema haya yote ni ziro tuâ¦,â alisema na kuongeza kwamba wakati anasoma, sekondari haikuwapo hata moja lakini sasa zipo shule zaidi ya 30. Alikumbusha namna ambavyo wana Chato walivyokuwa wakishonana kwenye mabasi.
âChato kilikuwa kijiji na leo ni wilayaâ¦umeme Chato haukuwepo, na sasa hivi tumeunganishwa na gridi ya taifa,â alisema na kuongeza kuwa umeme unapelekwa kwenye kila kata. Akisisitiza kuwa wanaelekea mbali kimaendeleo, Magufuli alisema si vyema kwa Mtanzania aliyeishi nchini akaanza kuzungumza kuwa hakuna chochote bila kukumbuka hata uwapo wa amani. âWengine wanasema usihubiri amani.
Amani nitaihubiri siku zote,â alisema. Aliomba Watanzania wanaoipenda nchi kuhubiri amani na kusema inafahamika nchi zinapokosa amani, hali inakuwaje. Alitoa mfano wa Uganda, Kenya baada ya uchaguzi na Sudan ya Kusini.
âNdiyo maana mimi nina hofu ya Mungu, namuogopa Mungu na Watanzania,â alisema. Hata hivyo alisema pamoja na mafanikio hayo, zipo changamoto. Alisema anataka ashushe zaidi umasikini, ikiwa ni pamoja na kudhibiti ushuru kwa wazalishaji wadogo wakiwemo bodaboda na mama lishe.
âNataka watanzania walipe kodi, wakubwa walipe kodi, wa kati kati walipe kodi, na wa chini walipe kodi kidogo,â alisema. Viwanda Aliendelea kusisitiza kuwa anataka Tanzania iwe ya viwanda itakayotoa ajira kwa vijana.
Alisema wataletwa wawekezaji kutoka nje na wa ndani watapewa fursa bila kuwekewa vipingamizi. Alisema waliobinafsishwa viwanda waviendeleze bila kufanya hivyo, moto wao uko karibu kwa kuwa watanyangâanwa. Alitoa mfano wa kiwanda cha nguo cha Mwatex cha mkoani Mwanza.
Wakulima, wafanyakazi Alisema atahakikisha bei ya pamba anaipandisha. Kuhusu mishahara ya wafanyakazi, alisema itaboreshwa kwa kuhakikisha wanapunguza makato yasiyo ya msingi. Alisema pia wafanyakazi wanaofanya kazi katika mazingira magumu, wataangaliwa. Pia ataangalia utofauti wa mishahara baina ya wafanyakazi.
Alisema yeye ni rafiki wa wafanyakazi wanaofanya kazi na sio wale wanaokosea mahali na kuhamishiwa maeneo mengine. âKwangu hakuna hama hama⦠utahamishwa tu kwamba unahama kwenda kufanya kazi kama kawaida na si kuhamishwa kwa sababu umekosea… najua wafanyakazi wengi ni wazuri. Wabaya ni wachache.
Najua wengine wamekuwa wakipita na kusema Magufuli ni mkali mno kwa wafanyakazi,â alisema. Alisema hana tatizo na wafanyakazi kwa kuwa amewahi kuwa katika nafasi hiyo ikiwamo kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Sengerema.
âNimeuza maziwa, nimechunga ngâombe, nimeuza furu..,â alisema na kuongeza kuwa pia atakuwa rafiki wa wakulima. Wavuvi Alisema ushuru wa mitumbwi utashushwa. Alisema itaanzishwa pia mipango mizuri ya kufuga samaki kwa kuleta utaalamu.
Alitoa mfano wa nchi ya Vietnam kwamba inaongoza kwa kuwa na utaalamu wa kufuga samaki. âWanaonipiga vita ni wale mafisadi wanaoogopa jeuri yanguâ¦ndiyo maana mliona nilipoteuliwa tu kupeperusha bendera ya CCM wamekimbia.
Wanafahamu nitawafunga magufuli,â alisema na kusisitiza kuwa atakuwa Rais wa Watanzania asiyebagua vyama, dini wala makabila. Hakuna bure Aliwaasa vijana kutambua kwamba hakuna vitu vitakavyokuja bure.
Alisisitiza umuhimu wa kuwaambia ukweli wananchi huku akitolea mfano wa mgombea ambaye aliahidi kuwa akiwa rais, ndani ya siku chache atahakikisha nyumba zote za nyasi zinatoweka.
Katika mkutano huo, msemo wa âMcheza Kwao Hutuzwaâ, ulidhihirika, kwani kwenye Uwanja wa Michezo ujulikanao kama Uwanja wa Mama Zaina ulifurika mno, ukikusanya idadi kubwa ya watu kwenye mji huo wa nyumbani kwa Dk Magufuli.
Magufuli, ambaye ni Waziri wa Ujenzi, alifika nyumbani kwake juzi akitokea mkoani Kigoma . Tangu kampeni zianze, mgombea huyo ameshafika mikoa 13 na kuomba kura katika majimbo yote.
Ikiachwa mkoa wa Kigoma ambako Dk Magufuli alihitimisha kampeni zake katika Wilaya ya Kakonko kabla ya kuja Chato, mikoa mingine aliyokwishakamilisha kampeni ni Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara, Morogoro, Tanga, Mara, Simiyu na Tabora.
Recent Comments