MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Massaburi amesema mabadiliko yanayonadiwa na vyama vya upinzani yalianza kuletwa na marais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya Uhuru.
Aidha, aliwataka Watanzania wasikubali kutekwa na vyama hivyo kwa kauli za uongo kuwa vitaleta mabadiliko mapya katika taifa la Tanzania, kwa kuwa tayari yalikwisha anza kufanyiwa kazi.
Aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kampeni za ubunge wa jimbo la Ubungo, zilizohutubiwa na mgombea wa CCM, Dk Didas Massaburi katika viwanja vya shule ya msingi Mwongozo Kata ya Makuburi.
Akizungumza katika mkutano huo, alisema baada ya Uhuru, Mwalimu Nyerere aliweka misingi imara ya watanzania kujitawala na kutaifisha njia kuu za uchumi zimilikiwe na wazalendo, hatua iliyojenga heshima ya Watanzania, kujenga umoja, mshikamano, amani na utulivu.
Alisema baada ya hapo mabadiliko yaliendelea kufanywa na marais waliofuata, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ambaye serikali yake imeleta mabadiliko mengi ya maendeleo kwa Watanzania, yasiyoweza kusahaulika.
âNadhani mnakumbuka ajenda yake ya kwanza baada ya kuingia madarakani ilikuwa ni kupambana na ujambazi uliokuwa umekithiri sana wakati ule, alileta mabadiliko kiusalama. Lakini pia aliboresha maslahi ya polisi na wanajeshi na kuboresha vituo vya polisi na makazi ya polisi na wanajeshi na kuyafanya ya kisasa.
Hayo ni mabadiliko piaâ. Alisema, sekta ya miundombinu nayo imefanyiwa mabadiliko makubwa baada ya barabara nyingi nchini kujengwa kwa kiwango cha lami, hivyo kurahisisha usafiri.
âWanaotoka mkoani Mara ni mashahidi, awali ili mtu afike Musoma alilazimika kupitia Nairobi na ili kufika Kagera ililazimu kupita jijini humo pia halafu uelekee Kampala ndio uingie Bukoba; lakini usumbufu wote huo umekwisha baada ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko hayo,â alisema.
Alisema, mbali na hayo, ilimlazimu msafiri aliyekuwa akienda Lindi na Mtwara kutumia wiki nzima barabarani
Recent Comments