HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imetumia zaidi ya Sh milioni 500 kupambana na kipindupindu tangu kilipozuka Agosti 15 mwaka huu.
Hadi sasa watu 1194 wameugua ugonjwa huo katika Manispaa hiyo na 17 wamefariki dunia.
Akizungumza baada ya kupokea msaada wa dawa na vifaa tiba uliotolewa na Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mussa Natty, alisema kila siku kuna wagonjwa wapya wanaripotiwa na jana walikuwa 15.
Msaada huo wenye thamani ya Sh milioni 15 ulitolewa na benki hiyo kupitia sera yao ya kurudisha faida kwa jamii katika Wiki Maalum ya Huduma kwa Wateja inayoadhimishwa na benki hiyo kila mwaka.
âNi gharama kubwa sana kumuhudumia mgonjwa wa kipindupindu, katika kila nyumba anayotoka mgonjwa lazima tumwage dawa nyumba 10 zinazomzunguka, tumetoa sana elimu lakini hali bado si nzuri na kesho (leo) tutakutana na wenyeviti wote kuangalia namna ya kudhibiti ugonjwa huu,â alisema Natty.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema Wiki Maalum ya Huduma kwa Wateja itaadhimishwa Oktoba 5 hadi 11 mwaka huu katika matawi yote ya benki hiyo Tanzania Bara na Visiwani.
Naye Herieth Faustine anaripoti kuwa katika Manispaa ya Temeke wameripoti wagonjwa 211 huku Ilala kukiwa na wagonjwa 968, hali iliyosababisha manispaa hizo kupiga marufuku uuzwaji wa vyakula holela ikiwa ni jitihada za kupambana na ugonjwa huo.
Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, David Langa alisema jana kuwa idadi hiyo imekuwa ikiongezeka na kwa jana walipokelewa wagonjwa 28 kutoka katika kaya tofauti ndani ya manispaa hiyo.
Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on.
Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com
Recent Comments