MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, ameahidi atakapochaguliwa atahakikisha anafunga mapigano kati ya wakulima na wafugaji huku akihadharisha viongozi atakaowateua kuwa lazima wahakikishe hayatokei kwenye maeneo yao.
Magufuli ambaye alikuwa akihutubia jana katika eneo la Kibaigwa wilayani Kongwa katika Mkoa wa Dodoma, amesema viongozi atakaowateua kuanzia makamanda wa polisi, wakuu wa wilaya na mikoa, wawe macho vinginevyo, ikitokea mapigano katika maeneo yao, hawatakuwa na kazi.
âViongozi nitakaowateua wawe wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, katibu tarafa, makamanda wa polisi wa mikoa, wakuu wa polisi wa wilaya ikitokea mapigano kwenye eneo lake, siku hiyo kazi anaondoka nayo,â alisema Magufuli.
âHaiwezekani watu wakawa wanauana na hao viongozi niliowateua wakakaa na kula upepo,â alisisitiza na kuongeza kwamba inawezekana wachache wasimpende, lakini akaomba wananchi wa Kibaigwa wamchague aweze kutekeleza ahadi zake.
âNa mje mniulize kuwa Magufuli ulisema utakomesha mapiganoâ¦mbona yametokea,â alisema na kusisitiza kuwa haiwezekani awe rais mapigano yawepo na watu waendelee kufa. Alisema anachotaka ni kuona watanzania wote wakiishi kwa amani.
âHakuna mtanzania daraja la kwanza na mtanzania daraja la piliâ¦na haya machoko choko ndiyo yanavunja amani. Naomba ndugu zangu wa Kibaigwa mniamini kweli, nataka kufanya kazi,â alisisitiza na kusema ndiyo maana anaposimama kwenye majukwaa hatukani wananchi wa vyama vingine.
Akihutubia maelfu ya watu waliohudhuria mkutano huo wa kampeni, Magufuli alisema, mapigano kati ya wakulima na wafugaji, ni miongoni mwa mambo yanayomuumiza. Katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, Dk Magufuli aliwaomba watu wa makabila yote waishi kwa amani.
Alisema anataka kuona wakulima wanalima kwa wingi vivyo hivyo wafugaji wakifanya shughuli yao kwa ufanisi. Alisema kama maeneo yamepungua ya kulima na kufuga, Rais anao uwezo wa kutafuta eneo lingine na kuwaweka watu.
Alitaja Sheria namba 4 ya ardhi ya mwaka 1999, Sheria ya Vijiji ya mwaka 1999 na Sheria ya Matumizi bora ya ardhi ya mwaka 2007, zinampa rais mamlaka hayo. âKatika mambo yanayoniumiza ni pamoja na mapiganoâ¦inachosha kuzika na kupigana,â alisema Magufuli.
Akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai, alimuita shujaa kwa kukemea mauaji yaliyotokana na mapigano ya wafugaji na wakulima.
OP Mtanzania
Recent Comments