Recent Comments

kutoka viwanjani

By ObyMack David Nov 5, 2015

Wageni mbalimbali wanaendelea kuwasili hapa uwanjani.

Wameingia marais wastaafu akiwemo Benjamin Mkapa,Ally Hassan Mwinyi na wake zao,mawaziri wakuu wastaafu Msuya na wengineo,Jaji Augustino Ramadhan na sasa jaji mkuu Othman Chande anaingia na ndio atamuapisha rais mteule.

Marais saba wa nchi mbalimbali wanahudhuria tukio hili. Pia waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga yupo

Wapo mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa jumuiya za kimataifa na mashiriki ya UN.

Spika wa bunge Anne Makinda na naibu spika Job Ndugai wamo.

Rais wa Zanzibar na delegation yote ya Zanzibar akiwemo Pandu Ameir Kificho wamehudhuria.

Watu ni wengi kweli kweli

RAIS MTEULE KATIKA KILA TUKIO MUHIMU MVUA ILINYESHA IKIWEMO LEO. ISHARA YA BARAKA NA UTAWALA HALALI WA RIDHAA YA WANANCHI.

Vikosi vya majeshi ya wananchi ya tanzania viko tayari kwa gwaride maalum.

Wabunge wateule wa Jamhuri ya Muungano wameshaketi tayari.

Jaji Mkuu Othman Chande ndio anawasili sasa hivi.

Bendera ya Rais wa sasa itashushwa na kuashiria ukomo wa serikali ya awamu ya nne na Rais wa awamu ya tano atakapoapishwa bendera ya taifa itapandishwa.

– Anaingia mke wa Rais Mteule Mama Janet Magufuli

– Wapo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa

– Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amewasili hivi punde

– Rais Jakob Zuma wa Afrika Kusini pia naye amefika.

-Maandamano rasmi ya kuelekea Jukwaa Maalum la Kuapishwa Rais mteule yataongozwa na Jaji Mkuu,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu Mkuu Kiongozi.