Mara nyingi wasomi wengi hasa hasa wale waliokuwa wakifanya vizuri darasani kuliko wengine, wengi wao wanamaisha ya kawaida licha ya kuwa na mshahara mnono pamoja na marupu rupu ya kutosha,
Si hapo tu,
Bali hata katika utendaji ufanisi wao ni wa kawaida sana ukilinganisha na wale walio kua medium au moderate performers mashuleni au vyuoni,
Mifano ipo mingi sana but nitaweka michache tu,
Mzee BAKHRESA anautajiri mkubwa sana na kila kukicha anazidi kupanua wigo wake wa kibiashara kwa kuongeza biashara zingine . Alianzia kuuza unga wa ngano kisha kapanua wigo mpaka kwenye biashara ya vinywaji n.k,
Pale UDSM ambapo tunaaminishwa kuwa ndio chuo bora kabisa nchini kuna maprofesor waliobobea kwenye masuala ya biashara na masoko lakini bado wanamaisha ya kawaida wana pesa ya mboga tu, na wanategemea teuzi kutoka kwa viongozi wa serikali ambao miaka kadhaa iliyopita walikuwa ni moderate students,
Tizama taasisi zinazo simamiwa na watu waliokuwa vipanga mashuleni zina hali gani mpaka sasa,
(Utapata jibu sahihi tumia mifano hai),
Sababu ni hii hapa
Unatakiwa uelewe concept mbili ambazo ni MEMORY na THINKING
Memory ni kumbu kumbu na Thinking ni kufikiri/ kutafakari
Ili ufauru mtihani unahitaji MEMORY (kukumbuka kile ulichokisoma), vipanga hufaulu kwa kuwa na uwezo mzuri wa KUKUMBUKA kile walicho kisoma,
Pengine walikuwa vipanga kwa sababu walirudia rudia mara nyingi kusoma kile walichofundishwa,
THINKING (Kufikiri) ndiyo chanzo cha tatizo na ndio sababu inayofanya wasomi wengi kuwa na maisha ya kawaida na kipato cha chini ,
Matajiri wengi ni watu wenye elimu ndogo wanao umiza vichwa usiku na mchana kufikiria na kubuni mbinu za kuwaongezea kipato na kuboresha utendaji ,
Chukua muda kutafakari kwa nini watu wengi wenye GPA nzuri sana lakini hupigwa chini na watu wenye GPA ndogo ktk interview ,
Jibu ni kuwa kinacho angaliwa ni uwezo wa kufikiri na sio kumbu kumbu.
Tujijengee mazoea ya kufikiria na kutafakari.
HUU NDIO UGONJWA UNAO WASUMBUA WAHITIMU WA UDSM,
Karibuni tupigane kwa hoja.
Recent Comments