simamia.com
Kijana mmoja ambaye alikuwa Daktari alimposa binti mmoja ambaye alimpenda sana na ndoto yake ilikuwa ni kuishi nae tena kwa Maisha ya amani na furaha tele.Sasa kuna kitu kimoja kibaya sana ambacho binti aliapa kutokubaliana nacho hata kwa ncha ya upanga,binti huyo hakumpenda hata kidogo mama wa kijana ambaye alikuwa amepanga kuoana nae,alimchukia kama kinyesi kisichofaa hata kutazamwa eti kisa alikuwa ni bibi kizee,mchafu tena hana hata ile hadhi ya kuitwa mama wa mtu furani.Binti kwa kulitambua hilo aliamua kumuita kijana huyo na kumwambia: “Unasikia ,mama yako simpendi na sitaki kumuona hata kwenye harusi yetu,nenda kamwambie asikanyage kabisa ndani ya uwanja wa harusi yangu Maana ni mchafu na tena hafai,
Sasa chagua moja ima unioe Mimi au ukakae na mama yako huyo.Mimi sitaki kuwa na mama mkwe mchafu kiasi hicho na anayeonekana kama mchawi”. Yale Maneno yalimchanganya sana kijana na kumuacha akiwa ndani ya njia panda asijue hata cha kufanya.Kichwa chake kilimuuma sana Maana mama yake hakutaka amuache njia panda na alimhitaji ,,,vile vile hata binti mwenyewe alimpenda sana.Sasa Katika kufikiria sana aliamua kumtafuta mwalimu wake aliyemfundisha somo la Sayansi pindi alipokuwa darasa la saba,aliamua kufanya hivyo kwa sababu alimtambua vyema mwalimu wake huyo Kutokana na moyo wa busara aliokuwa nao.Katika kumtafuta hatimaye alifanikiwa kumpata na moja kwa moja akamwambia:
” Mwalimu nipo ndani ya njia panda na mpaka hapa nilipo sijui hata nifanye nini.Kuna binti nampenda sana na nimeamua kumuoa ila Kiukweli amenipa masharti ambayo yamenivunja moyo sana.Katika hayo masharti aliniambia kama nataka kumuoa yeye na kuishi nae kama Mme na mke basi lazima nikubali kuachana na mama yangu na nimtelekeze kabisa, Sasa mama yangu nampenda sana na bado namhitaji japo amezeeka na kuchoka sana,vile vile hata binti ninayetaka kumuoa nae nampenda sana na sitaki kumuacha sasa naomba unishauri nifanyaje?”.Yule mwalimu alitabasamu kisha akamwambia, “Nenda kaitazame mikono ya mama yako ilivyo na hapo ndipo utakapotambua nini cha kufanya”. Kijana aliupokea ushauri ule na akaamua kuufanyia kazi.
Alirudi kwa mama yake akamuomba amuonyeshe mikono yake ili aichunguze.Sasa Wakati ameishikilia mikono ya mamae alijikuta akipigwa na butwaa Mara baada ya kuikuta ikiwa imejaa ukurutu ,vidonda na viganja vyake vilikuwa na kila dalili za kuumia.Alipomuuliza kwa nini mikono yake iko hivyo, mama yake akamwambia,” Mwanangu usinione nipo hivi,nimeteseka sana kwa ajili yako.Baba yako alifariki na kukuacha ukiwa mtoto mdogo wa miaka miwili tu,nilizunguka huku na huko kutafuta ridhiki kwa ajili yako,nimefanya sana vibarua vya mashambani na nimeponda sana kokoto ili wewe upate kusoma Mwanangu. Sasa kiufupi ni hivyo tu,wala usishangae sana kwa nini mikono yangu ipo hivyo “.Kijana alilia na kuhuzunika sana huku akijisemea ,” Kumbe mama yangu ni wa thamani hivi Katika Maisha yangu, Kumbe isingekuwa yeye hata huu udaktari nilio nao nisingeupata? Ee Mungu naomba umbariki mama yangu huyu na unisamehe kwa yote niliyokuwa nikitaka kuyafanya kwake”.
Kuanzia siku ile Kijana akimpigia simu yule binti akamwambia uchumba wao umevunjika kwa sababu ya tabia yake ya kutokumpenda mama yake.Aliahidi kumtunza na kumjali mama yake mpaka pale anakapoondoka duniani, aliitambua thamani yake na ndio maana aliusimamia huo msimamo. Kama nikumpata mke mwema aliamini atampata tu maana wanawake wapo wengi duniani na wanazaliwa kila uchao,tofauti na mama ambaye yeye ni wa pekee Katika dunia na ukimpoteza hautampata tena.
===>Sasa na wewe leo ichunguze mikono ya mama yako ili uyagundue Magumu yote aliyoyapitia na kukufikisha hadi hapo ulipo.Huenda baba yako alimtelekeza mama yako ungali mdogo lakini yeye hakukata tamaa kukulea na kukutunza hadi hapo ulipopafikia.Kumbuka usikubali kamwe kumsaliti mama yako au wazazi wako kwa ujumla eti kisa ya mchumba wako uliyenae,simamia msimamo wako wa kutowatelekeza wazazi wako ili Mungu wa mbinguni akubariki na kukupa Maisha marefu na yenye amani hapa ulimwenguni.
Recent Comments