Imebainika kuwa msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu ameamua kuingia kwenye muzuki wa Bongo Fleva. Prodyuza kutoka MJ Records, Daxo Chali ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa Wema Sepetu ameshiriksha katika wimbo wa Haitham ambao unatoka kesho, na kubainisha kuwa Wema ni muimbaji mzuri. Daxo ameeleza kuwa awali alitaka wimbo huo afanye mwenyewe Haitham na ulipokamilika aliona kuna haja ya mtu mwingine kuwepo katika ngoma hiyo ingawa alisita kutokana Haitham wimbo wake wa kwanza alimshirikisha Mwana FA hivyo watu wataona anabebwa lakini alipokaa na kuweza aliona Wema anafaa ndipo wakamtafuta. âKuna siku kweli akaja, so tukamuingiza studio tukamuonyesha mashairi aingize wala hakusumbua, kwanza Wema anajua kuimba sema watu wengi hawajui ilo suala ila kitu kilichokuwa kinamsumbua sana ni zile melodi kwa sababu ile ngoma. ni ya kiswahili lakini imeimbwa kama kifaransa, so ndio kitu kilichokuwa kinamsumbua sana ni kutamka yale maneno lakini kwenye kukaa kwenye key yupo vizuri sana,â
Kwa jina anaitwa Shaban Rashid Said Kisleu na ni mhariri hapa Simamia Media Group.
Natumaini mtafurahishwa na yake nitakayowaletea na mtaendelea kufatilia mitandao wa Simamia.com
Kumfikia, tuma email SimamiaTeam@gmail.com
Delete wema
Delete wema
Zepetu wema.