Zifuatazo ni sababu kadhaa ambazo ‘ Watafiti ‘ hawa wameziorodhesha ambazo zinaashiria tabia za Wanaume na Vijana wa siku hizi ambazo zimeondoa ule Uanamume / Ubaba / Ujana wao kiasi cha hata ‘ kuwasikitisha’ Wanawake / Mabinti wengi:
Kutukuka kwa ‘ umbea ‘ na kukubali ‘ Kutawaliwa ‘ na Wapenzi wao nyumbani
Kutukuka kwa kupiga ‘ selfies ‘ sana
Kutukuka kwa Kuvaa Suruali zao halafu wanatuachia wazi ‘ makalio ‘ yao
Kutukuka kwa kupenda ‘ Kujiremba ‘ kuliko Dada / Mama / Wake / Mademu zetu
Kutukuka kwa kutokuwa ‘ Wasiri ‘ hasa kwa mambo yetu ya ‘ Faragha ‘
Kutukuka kwa kula Chips, mikate ya Siagi na Jam, Mayai ya Kukaanga na ‘ Soseji ‘
Kutukuka kwa kutoweza kuwafikisha ‘ Vileleni ‘ Wapenzi wao
Kutukuka kwa wengi wao kupenda kubana sauti pale wanapokuwa wanaongea
Kutukuka Kwao kwa kupenda Kuvaa mavazi ‘ yanayobana ‘ wanaita ‘ Vimodo ‘.
Kutukuka kwa Kuvaa ‘ hereni ‘ masikioni na ‘ Kusuka ‘ nywele zao
Kutukuka kwa kupenda Kukaa muda mrefu na Watoto wa Kike kuliko wa Kiume
Hizi ni baadhi tu ila ‘ yamesemwa ‘ mengi na hawa ‘ Watafiti ‘ hivyo ili ‘ usinichoshe ‘ au ‘ tusichoshane ‘ sana tafadhali kama unataka ‘ Kujijua ‘ kama Wewe mwana JF ( Mwanaume ) una tabia za Kimama mama / Kike Kike au upo kama akina sisi ( GENTAMYCINE ) wenye tabia za Kibaba Baba / Kiume Ume basi tafuta ‘ Kopi ‘ yako ya MWANANCHI au ingia zako tu MWANANCHI online uweze kusoma kila kitu.
Recent Comments