Jarida la Reddit liliwauliza wahudumu wa mashirika mbalimbali ya ndege kuhusu huduma zipi ambazo abiria wanaweza kuwa wanapatiwa lakini hawaziombi wawapo safarini.
Kuanzia pombe za bure mpaka dawa kama utaumwa ghafla, hivi ndio vitu nane ambavyo usisite kuomba ukiwa kwenye ndege kwa mara nyingine.
1. Chupa nzima ya soda
Wahudumu wa ndege huwa wanabania sana kutoa soda, kwa mara nyingi kukupa nusu tu ya chupa wakiichanganya na barafu ili ionekane nyingi lakini haitoshi kukata kiu. Kwahiyo mara nyingine ukifanyiwa hivi, agiza chupa nzima. Wahudumu wa ndege mara zote wanafanya utakachowaambia, na kama hawatakuwa na akiba ya kutosha, watajaza tena glasi yako.
2. Dawa na bandeji
Ingawa inategemea sana na taratibu za Shirika la Ndege husika, ndege nyingi zinakuwa na dawa za msingi kama vile za kutuliza maumivu na kutuliza kiungulia pamoja na bandeji. Hivi vyote hutolewa bure unapohitaji.
3. Chokoleti ya moto
Kama mbadala wa chai au kahawa, mashirika mengi yanakuwa na chaguo la kukupa chokoleti ya moto. Mashirika ya ndege ya Etihad, Virgin Atlantic, na Southwest Airlines ni baadhi tu ya yale yanayotia huduma hii hata kwa madaraja ya kati.
4. Pombe ya bure
Kwakuwa kimsingi nauli yako ya ndege siku hizi inajumuisha huduma zote utakazopatiwa, wengine hudhani hii inajumuisha na pombe pia. Hata hivyo, makampuni mengi ya ndege bado yanatoa pombe za bure mpaka sasa.
Kwa mfano Shirika la Ndege la Alaska bado linatoa huduma ya pombe za bure kwa baadhi ya safari zake; Shirika la Ndege la Marekani (US Airways) linatoa waini ya bure pamoja na chakula cha usiku kwa ndege zake zinazofanya safari za kimataifa; Mara nyingi hii inafanyika kwa ndege zinazofanya safari ndefu sana zinazochosha au kwa zile zinazofanya safari za kimataifa.
5. Mikoba yenye vifaa maalumu
Kwa ndege za masafa marefu, baadhi ya makampuni huweka kwenye akiba yao vitu kama vizuia sauti vya masikio, peni, chanuo za nywele na karata ambavyo utakopoomba utapatiwa mara moja. Ndege za kampuni ya Emirates ina mikoba yenye vifaa hivi ambapo wanaweka vifaa vya bure vya kunyoa, miswaki, soksi na karata kwa ajili ya kukufanya usichoke sana kwenye safari ndefu.
6. Kuongezewa vitafunwa
Vitafunwa kidogo vinavyotolewa kwa abiria kwenye ndege havitoshi na mara nyingi huwa havishibishi, vinakuacha ukiwa na njaa vile vile. Cha kufanya ni kuomba uongezewe tu â kama kuna vitakavyobakia baada ya abiria wote kuhudumiwa, wahudumu wa ndege mara zote huwa wanakuongezea kwa furaha kabisa ili mteja wao uridhike.
7. Kuangalia chumba cha marubani
Kwa kawaida chumba cha marubani kwenye ndege huwa kinafungwa muda wote na muda pekee wa abiria kumsikia rubani wenu ni mwanzo wa safari, mwisho wa safari au ikitokea hitilafu ya kiufundi au hali ya hewa ikiwa mbaya mnapokuwa angani. Lakini kama ukiwa unataka uone jinsi chumba hiki kilivyo, muombe mhudumu wa ndege na yeye ataomba ruhusa kwa rubani ili uweze kwenda kuangalia mitambo ya kuongozea ndege ilivyo kwenye chumba hicho maalumu.
Recent Comments