KAMA wasemavyo Waswahili, dunia ina mengi⦠leo nimeamini, si kwa kituko hiki. Kisa si kisa, labda ni kisasi, sijui!
Basi bwana kama kawaida, nimeamka asubuhi kuwahi katika kibarua changu kilekile cha kuchanganya zege ghorofa lipande. Ila usimwambie mtu siri hii kwa sababu âwifeâ anajua nafanya kazi kitengo maalumu pale ikulu. Wanawake bila uongo hawaendi, nani atakubali kuolewa na mkoroga zege mjini hapa?
Nisipotee katika lengo, tujikite katika mada. Wakati napanda daladala tulikuwa watatu tu, lakini tulipigana vikumbo almanusura kuuvunja mlango wa wenyewe, hivyohivyo kibishi nikafanikiwa kuzama ndani. âMtoto wa mjini hakosi sitiâ, nikapata moja ya dirishani, kisha taratibu nikaweka nyau chini.
Safari ikaanza, taratibu, taratibu, kama msafara wa wahenga! Dereva anaendesha, abiria wanaendeshwa na konda naye, anakusanya masurufu yake.
Wakati konda anaendelea kukusanya nauli zake, ndipo alipomfikia bwana mmoja barobaro kajaza misuli, kwa jina yu-aitwa Dizasta! Jina lake tu maajabu! Uchuro huu. Ptuuuuuh!
NINI KIKATOKEA?
Jamaa yule akagoma kulipa nauli, japokuwa sura yake hata bila kutumia âkaboni fotiniâ iliashiria kabisa alikula chumvi nyingi na bila shaka ni mhusika katika kamati ya wahenga.
Konda kuona jamaa hakubali kulipa nauli akafoka, âsijaja kucheza hapa, we bwana nitakupasua!â
Jamaa naye akajibu, âKausha basi nitakupa shilingi mia mbili, mi mwanafunzi!â
Watu wote tukashangaa, wengine wakacheka hata vicheko vikamkera sana mhenga huyu. Kwa jazba akajizoazoa katika kiti chake, akasimama na kuanza kulalamika kwa hisia,
âMimi ni mtoto mdogo sana, mnanionea! Mnanionea!â aliendelea kulalamika, âBasi kama hamuamini, ngojeni basi niwavulie muone kama sina maâ¦â Kabla hajamaliza, konda akadakia,
âTutajuaje kama umenyoa?â
Wote tukaangua kicheko! Jamaa akakasirika, akakamata mkanda wa suruali yake ili asaule, kuona hivyo, akina mama wa pwani waliojaaliwa busara, hekima na huruma, wakamwahi, wakambembeleza, âBasi baba, basi baba inatosha, usifanye hivyo utajidhalilisha⦠basi baba, usilie wala usisaule.â
Safari bado inaendelea hapa, namuona kakaa anakunywa soda na biskuti tulizomnunulia ili kumbembeleza, asilie wala asisaule!
Recent Comments