Kila siku watu wanatengeneza pesa kupitia filamu nchini Marekani, watu wanatajirika na hivyo kuzifanya filamu zao kununuliwa sana kila kona duniani. Hapa, nitakuwa nikikuletea uchambuzi mbalimbali wa filamu, takwimu, mapato na mambo mengine mengi kuhufu filamu.
Kwa leo tuanze na mambo machache kuhusu filamu, nitakwenda kuwaambia kuhufu filamu zilizoingiza pesa nyingi kwa wikiendi hii ya juzi, uone jinsi watu wanavyoingiza pesa kupitia majumba ya sinema duniani.
Filamu iliyoingiza kiasi kikubwa cha pesa kwa wikiendi ni Dunkirk. Filamu hii imerekodiwa na Warner Bros, imeingiza dola milioni 26,611,130 (Sh. Bilioni 52) Imeonyeshwa katika majumba ya sinema 3748. Kwa wastani, kila jumba limeingiza kiasi cha dola 7100 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 14. Kwa ujumla mpaka sasa hivi filamu hiyo imeingiza kiasi cha dola milioni 101,317,350 zaidi ya shilingi bilioni 200. Bajeti yake ilikuwa dola milioni 100 ambazo ni zaidi ya bilioni 200. Bado inaendelea kuonyeshwa na inategemewa kuingiza pesa nyingi zaidi.
Namba mbili inashikwa na The Emoj Movie. Imerekodiwa na Sony. Imeingiza dola milioni 24,531,923 (Sh. Bilioni 49). Majumba ya sinema 4075. Kwa ujumla imeingiza dola milioni 24,531,923 (shilingi bilioni 48). Bajeti yake ni dola milioni 50 (shilingi bilioni 100).
Namba tatu ni Girls Trip. Imerekodiwa na Universal. Imeingiza dola milioni 19,646,305 (shilingi bilioni 39). Kwa ujumla imeingiza dola milioni 65,085,525 (shilingi bilioni 122). Bajeti yake ni dola milioni 19 (shilingi bilioni 38).
Namba nne ni Atomic Bronde. Imerekodiwa na Focus. Imeingiza dola milioni 18,286,420 (shilingi bilioni 38). Kwa ujumla imeingiza dola milioni 18,286,420 (Sh. Bilioni 38) bajeti yake ni dola milioni 30 (Sh. Bilioni 60)
Namba tatu ni Spiderman Homecoming. Imerekodiwa na Sony. Imeingiza dola milioni 13,261,372 (Sh. Bilioni 26). Kwa ujumla mpaka sasa imeingiza dola milioni 278,168,177 (Sh. Bilioni 556. Bajeti yake ni dola milioni 175 (Sh. Bilioni 350)
Spiderman Homecoming
Recent Comments