Mwanaume aliyejitambulisha kwa jina la Samson Segeli, amefunguka ya moyoni jinsi mkewe, Ester Gaspari alivyomkataa baada ya kuishi naye kwa miaka mingi na kuhangaika kumsomesha mpaka alipopata kazi ya ualimu wa shule ya msingi.
Segeli anaeleza kwamba alifunga ndoa na Ester mwaka 2003 katika kanisa la KKKT Boma na kuanza maisha ya kindoa, yeye akijishughulisha na biashara ndogondogo na mkewe akifanya biashara ya kuuza mkaa.
Segeli anaeleza kwamba kabla ya kumuoa Ester, alikuwa akiishi na mwanamke mwingine ambaye alizaa naye watoto watatu lakini baadaye, wazazi wa mwanamke huyo walimchukua binti yao kwa maelezo kwamba lazima Segeli amalize kulipa mahari ya ngâombe saba walizokubaliana.
Mgogoro huo uliendelea kwa muda wa miaka mitatu ambapo baadaye, Segeli aliamua kuoa mwanamke mwingine baada ya kushindwa kulipa mahari na hapo ndipo alipokutana na mwanamke huyo, ambaye kabila lake ni mchaga na mwanaume ni Mpare.
Mwanaume anaendelea kueleza kwamba baadaye, aliamua kumsomesha mkewe kwenye fani ya ualimu na baadaye akapata ajira kwenye Shule ya Msingi Shamaliwa iliyopo Igoma jijini Mwanza.
Baadaye, mwaka 2007 mwanamke huyo alianza kubadilika na mwaka 2010 alimpeleka mahakamani kwa madai ya talaka na kugawana mali, kisingizio chake kikubwa kikiwa ni kwamba mwanaume huyo anamletea watoto aliozaa na mwanamke mwingine nyumbani kwake, jambo ambalo hayupo tayari.
Mahakama iliamuru kwamba wawili hao warudi nyumbani na kuishi pamoja bila kuwabagua watoto lakini mwanamke huyo hakukubaliana na hukumu hiyo, akaamua kuondoka nyumbani kwake moja kwa moja.
Recent Comments