Watu wanne wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya kaliua- kigoma eneo la kazilambwa kata ya Usinge ambayo imehusisha basi la kampuni ya DMA lililokuwa likitoka jijini Mwanza kuelekea mkoani kigoma.
Kufuatia ajali hii ambayo imetokea jana jioni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya kaliua ABEL BUSALAMA amethibitisha kutokea kwa ajali hii ambapo amewataka madereva kuzingatia sheria za barabarani ili kuepuka matukio kama haya.
Dr ALISTIDES RAPHAEL ni mganga mkuu wa wilaya ya kaliua anabainisha hali ya majeruhi ambao wamelazimika kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya urambo kutokana na changamoto ya ukosefu wa hospitali ya wilaya hapa kaliua.
Nini maoni yako kuhusu tukio hili la kutisha watakie mapumzikomema hapo chini kwenye comment..
Kwa jina anaitwa Shaban Rashid Said Kisleu na ni mhariri hapa Simamia Media Group.
Natumaini mtafurahishwa na yake nitakayowaletea na mtaendelea kufatilia mitandao wa Simamia.com
Kumfikia, tuma email SimamiaTeam@gmail.com
Andeni Tanga Tanzania,
Allah awapumzishe salama walio poteza uhai wao na kuwaponya haraka majeruhi waweze kurejea uzima wao Inshaallah.
poleni saana mlipata matatizo hayo.