Na, Muhingo Mwemezi – Buhigwe
Ili kuondoa changamoto zinazowakabili Wananchi katika maeneo yao wanatakiwa kuwa na uchungu kwa kuwachagua Viongozi watakaoweza kutatata kero zao na si kupangiwa au kulazimishwa kuchagua Mtu wasiyemuhitaji kwa sababu zisizokuwa na msingi wakijua kama watafanya uchaguzi husi sahihi hawatapata maendeleo wanayoyakusudia
 Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo ameyasema hayo wakati akimnadi Mgombea Ubunge wa Chama hicho Jimbo la Buhigwe Mkoani Kigoma,Garula Kudra katika Kata ya Mwayaya ambapo amewataka Wananchi kuchagua Kiongozi wanaeona anaweza kuwaletea maendeleo kulingana na changamoto zinazowakabili
Zitto amesema Mashinikizo ya vyama hayatasaidia kutatua kero bali Kiongozi mwenye uwezo na utashi kwa wananchi huku akitoa Mfano wa uchaguzi uliofanyika mwaka 1995 ambapo wakazi wa Jimbo la Musoma Vijijini walipo mchagua mfuasi wa chama cha NCCR Magaeuzi aliyefahamika kwa jina la Poul Mdobo na maendeleo yalionekana
Amesema wanachi wanatakiwa kutambua kuwa Dunia inabadilika kila kukicha na inahitaji Watu wanaojitambua ambao wanaweza kushirikiana wao kwao huku wakifahamu maendeleo yaa Jimbo lao ni yao wenyewe na watatakiwa kuyatatua huku akimwombwa kura Mgombea wa ACT Wazalendo Garula Kudra kwa maendeleo
ââWapo watu wanaowatisha na kuwalazimisha Wananchi kutowapigia kura Viongozi wa Vyama vya Upinzani kwa Madai hawezi kuleta maendeleo, sasa nataka niwambie kuwa maendeleo hayawezi kuletwa na chama bali Viongozi bora wanapatika kwenye vyama hivyo Mtu bora anaweza kupatikana kwenye chama hata kama ni kidogo sana hivyo Wananchi amkeni, jitambueni zipimeni kauli za watu na vyama vyaoââamesema Zitto
Kwa upande wake Mgombea Ubunge amesema iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo yeye anatambua Kero zilizoko katika maeneo mbalimbali za Jimbo na wilaya ya Buhigwe na zinatofautiana huku akieleza yapo baadhi ya maeneo, kuna Vituo vya afya, lakini zipo kata nyingi ambazo wananchi wanatembea mwendo mrefu kufuata huduma hizo, kutokana na hali hiyo, ataishawishi serikali kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha kero ya kutembea mwendo mrefu   kufuata huduma hizo iznapungua.
ââNinatambua zipo kero kama upatikanaji wa Maji safi, Elimu Masoko ya Bidhaa za kilimo, ili wakulima waweze kupata tija katika kilimo kulingana na Garama wanazozitumia, hatua ambayo imekuwa ikichangia wakulima kukata tamaa katika kilimo nitatatafuta uwezekano wa Masokoââamesema Kudra
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Pilipo Mpango aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupelekea Jimbo hilo kuwa wazi na kutangazwa uchaguzi Mdogo ambao unatarajiwa kufanyika May 16, 2021
Mwisho
Recent Comments