Wiki ijayo, mataifa saba ya Afrika yanatarajiwa kuanza kufanya vipimo vya kinga ya mwili dhidi ya virusi vya corona, kituo cha Afrika cha kudhibiti magonjwa (CDC) kimeeleza .
Vipimo hivyo ni sehemu ya jitihada za kuweza kuelewa ukubwa wa mlipuko wa janga hili katika bara la Afrika.
“Liberia, Sierra Leone, Zambia, Zimbabwe, Cameroon, Nigeria pamoja na Morocco ndio mataifa ya kwanza ya Afrika ambayo yamejidhatiti kufanya vipimo hivyo, kiongozi wa CDC John Nkengasong ameeleza.
Alisema bara la Afrika imefanya vipimo vya corona milioni 9.4, idadi ambayo inakaribia milioni 10 ambayo ilikuwa imelengwa.
Dkt Nkengasong alisema Afrika imefanya jitihada nzuri katika kuanzisha chanjo.
Alisema jitihada za bara hili zilianzishwa na taasisi kadhaa ili kufanya jaribio na kuanza kutoa na kufadhili chanjo.
Afrika imerrikodi maambukizi 1,084,904 ya virusi vya corona, kwa mujibu wa takwimu ya chuo kikuu cha Johns Hopkins.
Recent Comments