NA, ANKO G.
Nishati ya umeme ni kichocheo cha maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla na katika siku ya leo nimekuandalia makala fipi inayo angazia ahadi ya serikali kutatua mgawo wa umeme nchini Tanzania tangu mwaka 2010 mapaka mwaka huu wa 2024.
Aliyekuwa Meneja Uhusiano TANESCO Badra Masoud alitangaza mgawo mkali wa Umeme wa siku 30 kuanzia Desemba 2010 na kuisha Januari 2011 tangazo ambalo halikuzaa matunda.
Na ilivyo fika Machi 2011 Badra Masoud alitangaza kuwa mgawo wa Umeme utaisha wwaka 2013.
Ilipo fika Juni 2014 aliyekua Katibu Mkuu wa wizara ya nishati na madini Eliakim Maswi alisema matatizo ya umeme yataisha mwaka 2025.
Ilipo fika Desemba 2014 Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO Jenerali mstafu Robert Mboma alisema mgawo wa uememe utaisha Machi 2015.
Ilipofikia Desemba 2015 Aliyekua Naibu waziri nishati na madini Dkt. Medard Kalemani aliiagiza TANESCO kuondoa upungufu wa umeme ifikapo Februari 2016.
Ilipofikia Desemba4, 2017 Aliyekua Waziri wa nishati na madini Dkt. Medard Kalemani alisema mgawo wa Umeme utaisha Desemba 15,2017.
Ilipofikia Machi 2020 Aliyekua Waziri wa nishati Dkt.Medard Kalemani aliagiza TANESCO kusitisha mgawo nchi nzima.
Ilipofika Machi 2021 Aliyekua Waziri wa nishati Dkt.Medard Kalemani alitoa siku 5 kwa TANESCO na Songas kuondoa tatizo la mgawo wa umeme.
Ilipofika Novemba 2021 Aliyekua Mkurugenzi wa TANESCO Maharage Chande alisema mgawo wa umeme utaisha mach 2022.
Ilipofika Mei2022 Aliyekua Mkurugenzi wa TANESCO Maharage Chande alisema matatizo ya umeme yataisha Novemba 2022.
Ilipofika Julia 2023 Aliyekua Waziri wa Nishati January Makamba alisema kuwashwa kwa mitambo ya bwawa la Nyerere (JNHPP) kutamaliza mgawo wa umeme.
Ilipofika Septemba 2023 Mkurugenzi wa TANESCO Mhandisi Isima alisema mgawo wa Umeme utaisha Machi 2024.
Ilipofika Septemba 2023 Rais Samia Suluhu alitoa Miezi 6 Kwa TANESCO kumaliza mgawo umeme.
Februari 2022 Naibu waziri wa nishati Judith Kapinga alisema mgawo wa umeme utaisha Februari 16,2024.
Ilipofika Februari6, 2024 Bunge lilipitisha azimio kuitaka serikali ihakikishe mradi wa bwawa la JNHPP Kuanza uzalishaji Februari 2024.
Ilipofika Februari 16, 2024 Naibu waziri wa nishati Judith Kapinga alisema mgawo utaisha Machi 2024.
Ilipofika Februari 16, 2024 Spika wa Bunge Dkt Tulia Akson aliipa serikali muda wa ziada miezi 4 hadi Juni 2024 kumaliza mgawo.
Je, unadhani ngawo wa umeme utaisha ifukapo June 2024 au unagonja ahadi nyingine ya kumaliza tatizo hilo nchini Tanzania?
Recent Comments