Waziri wa Fedha ameshauri mabadiliko ya tozo na kodi kwenye baadhi ya vitu. Kati ya vitu vilivyoshauriwa kufanyiwa marekebisho ni pamoja na vifuatavyo
–
Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye Dawa na Vifaa muhimu vinavyotumika kupima, kukinga, kutibu na kupambana na magonjwa ya mlipuko kama ugonjwa wa #COVID19
–
Hatua hii inalenga kutoa unafuu wa bidhaa hizo ili kurahisisha mapambano na udhibiti wa magonjwa hayo pindi yanapojitokeza
–
Bajeti ya 2020/2021 imependekeza kufuta tozo za mafunzo ya elimu kwa umma yatolewayo na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) yaliyokuwa yakigharimu Tsh. 250,000 kwa kila mshiriki. Imesema hilo ni jukumu la OSHA
–
Kama bajeti hii itapita, itaanza kutekelezwa kuanzia Julai 1, siku ambayo mwaka mpya wa fedha unaanza
Recent Comments