Klabu ya Soka ya Biashara utd kutoka Mkoani Mara jana imefanikiwa kupunguza uteja wa kufungwa kila mchezo hasa pale wanapokutana na klabu hiyo ya Simba.
.
Mpaka Sasa wamekutana mara sita katika Michezo mbalimbali huku Simba akifanikiwa kumfunga Simba kila wanapokutana kwa nyakati tofauti tofauti nyumbani na ugenini.
Mchezo wao wa leo haikuwa mechi rahisi, kila kitu kilikuwa sawa kwa Biashara katika nidhamu ya ukabaji na kila kitu kikawa sawa kwa Simba katika nidhamu ya ukabaji.
Ni kosa moja tu la Salum Kipaga ambalo pengine lingebadilisha taswira nzima ya mchezo bahati mbaya kwa Simba Bocco akashindwa kuuweka mpira wavuni na bahati nzuri kwa Biashara ambao pointi moja dhidi ya Simba ina maana kubwa sana kwao.
Timu zote mbili hazikuwa na ubora katika kutengeneza nafasi kwenye eneo la mwisho, Simba imekuwa na muendelezo wa kile tulichokiona dhidi ya Tp Mazembe, Yanga na leo mbele ya Biashara United.
Kama kuna sehemu ambayo walinzi wa Biashara United walikuwa na ubora mkubwa ni kucheza mipira ya juu na pia kuzicheza second balls karibu zote.
Kucheza dhidi ya John Bocco na Meddie Kagere ambao wana ubora katika mipira ya juu na katika kucheza second balls unahitaji uwe na ubora mkubwa wa kucheza dhidi ya ubora wao.
Kwa namna moja ama nyengine uwanja ulizinyima timu zote mbili fursa katika mipira ya counter attacks, zipo counter attacks kama mbili za Biashara ambazo kwa kiasi kikubwa zilikwamishwa na aina ya pitch waliyochezea hivyohivyo kwa Simba.
Game plan ya Simba ilikuwa ni kucheza mipira mirefu, nilielewa kwanini Gomes alimuweka Duncan Nyoni katikati ili kupiga mirefu kutokea chini ambayo mingi aidha ilichezwa na golikipa au kuchezwa na walinzi.
Hivyo kutokana na matokeo hayo kila mmoja ana kila sababu ya kutafakari ni wapi walipokosea ili wajirekebishe pale wanapoenda kwenye mechi zingine zilizo mbele yao, Pia kumbuka Ni vilabu ambavyo bado wanapigana kuhakikisha wanabaki kweye mashindano ya kimataifa ya CAF ….
Recent Comments