Tumeshazitazama sana video za hawa Jamaa wa Ghana wakicheza na majeneza misibani, fahamu tu kwamba hii ni kampuni rasmi na wanalipwa kufanya hivi na Benjamin ndie Mwanzilishi wa Kampuni hiyo, alianzisha hizi staili za kucheza ili kuondoa huzuni misibani ambako vilio hutawala zaidi kuliko kusherehekea maisha ya aliyetangulia.
Mteja anapofika kwenye Ofisi yao anapewa album ya picha ili achague staili gani ya mavazi anayoitaka ambapo Benjamin anasema sasa hivi biashara yake imekua kubwa na anapata muda mdogo sana wa kulala kwani tenda ni nyingi na sasa anawaza hata kufungua matawi ya ofisi yake kwenye Nchi nyingine.
Benjamin anasema pia kazi hii imetoa nafasi kubwa ya ajira kwani kwa sasa ameajiri Vijana zaidi ya 100 Nchini Ghana ambapo 95 ni wa kiume na watano ni wa kike, tazama zaidi simulizi yao kwenye hii video hapa chini.
Recent Comments