NA,ANKO G
Kata ya Kabanga (Makao makuu ya kata) ni miongoni mwa maeneo yanayo kua na kupanuka kwa kasi katika wilaya ya Ngara mkoani kagera ukilinganisha na mika kumi (10) iliyopita.
Hata hivyo kabanga eneo linalo chukuliwa kama mjini ni eneo lisilopungua kilomita 5 usawa wa barabara kuu inayo elekea Burundi Yani kuanzia eneo la Mlimani mpaka eneo la Mkagobero,mpaka wa Kijiji cha Ngundusi na Maeneo ya Kijiji cha Mrukukumbo.
Vilevile simamia.com imetembea baadhi ya maneo na kubaini kuwa maeneo mengi ya Kabanga hayana mpango miji ambapo watu hujenga wanavyo jisikia bila kujali mitaa kutoka nyumba hadi nyumba nyingine.
Pia simamia.com imeshihudia maeneo machache yakiwa yamepewa mitaa huku mingine ikionekana kuwa mipya.
Hivyo basi kwakua Kabanga ni mji unao kuwa kwa kasi simamia.com inashauri kuweka mipango miji mapema ili hata maeneo ambayo bado hayajajengwa yawe na barabara za mitaa kwaajili ya kuruhusu mawasiliano kwaajili ya usafirishaji pamoja na miundombunu ya maji na umeme.
Katika miji mingi maeneo ambayo leo yanaitwa uswahilini ni maeneo ambayo hapo awali hayakuwekewa barabara za mitaa ambapo leo maeneo hayo yanakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mafuriko na hata kushindwa kutatua majanga kama vile moto, magonjwa na mengine yanayo fanana na hayo.
Ni mhimu Baraza la aridhi la kata kwa kushirikiana na maafisa watendaji wa vijiji kuweka mipango miji katika maeneo yao kwani hii itasaidia kuchochea maendeleo kupandisha thamani aridhi na hata kuepusha migogoro ya aridhi.
Recent Comments