Recent Comments

BODABODA WA NGARA VAENI KOFIA NGUMU ACHENI MAZOEA

By Mwafrika Jan 9, 2024

Na mwafrika
Kwa utafiti wangu nilioufanya kupitia camera nene na simamia.com nimegundua na kujionea matatizo na ajari nyingi zinatokea ngara za bodaboda na hii ni kwa mujibu wa tafiti za simamia.com na camera nene.

Mwaka 2023 tuliamdika na kushauri dereva wa bodaboda wilayani ngara kuzingatia sheria pia tulishauri askari wa usalama barabarani kusimamia sheria barabarani lakini mwaka 2024 mambo ni yaleyale hasa kata ya kabanga.

Bodaboda wamekua wakiishi maisha wayatakayo barabarani na wakifanya wapendqvyo tena bila kuogopa wala kujali maisha yao lakini pia kubwa zaidi wengi wa waendesha pikipiki hapa ngara hasa kabanga hawavai kofia ngumu(element)sasa hii ji mbaya na ni hatari zaidi maana ikitokea ajari mambo yanakua mengine kabisa hata kupelekea kifo.

Simamia.com tunashauri tena na kuwaomba wasimamia sheria za usalama barabarani kusimamia ipasavyo bila kupepesa macho maana ngara inapoteza vijana na vijana wanapotea kwenye familia zao.

Ni kweli bodaboda imekua kimbilio la vijana wengi nchini na hapa wilayani Ngara ila sasa sheria hazifuatwi vizuri huenda mkazo unahitajika na Doris za kutosha huku elimu ya mara kwa mara itolewe maana wengi wa waendeshe pikipiki wanajifunza mtaani na ukute hawajui walifanyalo.

Mwisho kabosa simamia.com tunawaasa waendeshe bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani pia askari wa barabarani kusimamia na kuwakumbusha watumiaji wa vyombo vya moto kufuata sheria bila shututi.