Recent Comments

Boresheni Mazingira ya Shule Ili Mwanafunzi Aelemike Sio Kushirikisha Mwalimu Kwenye Siasa

By Baraka Bitariho Jan 12, 2024
Kumbe sio Kamera Nene tuu, Hata Simu Inahofiwa Kwani Mtaweza Kurekodi na kutaarifu Jamii Madudu Yanayoendelea Huku Tulipo. Ili shughuli iendelee kimya kimya, tumeona ni vyema tuwapore simu zenu mlangoni mlipokua mnaingia humu. Ila haijulikani kama nia ni kuondoa uhaba wa gesi uliopo ama ni kuhakikisha kama simu zetu ni za bei mbaya kuliko zile zenu. Angalau mgetupatia na vocha kama fidia ya kung'ang'anywa kwa simu zetu ambazo hamkutusaidia kuzinunua.
*PROPAGANDA ZA CCM KWA WATUMISHI WA SERIKALI (WALIMU)*
Imetokea siku za hivi karibuni kitengo cha propaganda ndani ya CCM  wamehamishia nguvu kubwa kwa watumishi wa serikali (hasa walimu) ambao wanadanganywa kwa vyakula na vinywaji kisha wanakusanywa mahala na kulazimika ama kusemekana ati wamemchangia hela ya fomu mgombea fulani.
This is totally wrong to our teachers in this country. Katiba yetu mbali na mapungufu yake inapiga marufuku watumishi wa UMMA kushiriki siasa katika masaa na maeneo ya kazi.  Lakini kwa wafuasi wa CCM hili limekuwa kama kicheko kwao maana wanaamua wanalolitaka wao na kwa muda wao.
Pokeeni mitungi ya Gesi Kama Mtanichukulia Fomu ya kuwania Muhura Ujao
Leo hii mbunge wa Ngara #Ndaisaba Ruhoro anawakusanya walimu wakuu na wakuu wa shule zote za serikali na binafsi Ngara nzima anawandalia  chakula vinywaji na hela za nauli kidogo, kisha inasemekana eti wamemchangia hela ya kuchukulia form ya kugombea uchaguzi ujao. Hili kwangu sio tatizo ila shida yangu katika hili ni tafakuri yangu baada ya matukio haya kama ifuatavyo;
Mosi, Walimu hawa wamehudhuria kikao hiki masaa ya kazi ambacho si kikao cha serikali bali kikao cha kirafiki katika mtazamo wa kisiasa (CCM) ili kuwezesha uhalali wa propaganda ya mgombea huyu katika uchaguzi ujao. Kiufupi walimu wameacha kazi wakaenda kikao cha kisiasa. Je, ni halali????
Kumbe sio Kamera Nene tuu, Hata Simu Inahofiwa Kwani Mtaweza Kurekodi na kutaarifu Jamii Madudu Yanayoendelea Huku Tulipo. Ili shughuli iendelee kimya kimya, tumeona ni vyema tuwapore simu zenu mlangoni mlipokua mnaingia humu.
Ila haijulikani kama nia ni kuondoa uhaba wa gesi uliopo ama ni kuhakikisha kama simu zetu ni za bei mbaya kuliko zile zenu. Angalau mgetupatia na vocha kama fidia ya kung’ang’anywa kwa simu zetu ambazo hamkutusaidia kuzinunua. Kama nia ni kupunguza uhaba uliopo, hata ununuzi wa vocha ni shida kweli, tusaidie kwa vocha basi kama kweli umethamilia kutatua shida zilizopo. Umeona tumeshindwa kujinunulia mitungi ya gesi, ila unaamini kweli tutakua na pesa ya kukuchulia fomu ya kuwania ubunge muhula ujao huku gesi, na nauli za kufika hapa umetuonea huruma na kutupatia. Ile fomu ya kugombea ubunge ndugu yangu itahitaji hela na sio kwenda pale na meno yetu meupe kama choki tunazozitumia huku mashuleni.

 

Pili, Ilani ya CCM, na hata sera za mbunge (huyu huyu) zilisemaje kuhusu uboreshaji wa elimu katika nchi hii na hasa kwa wilaya hii (Ngara) na kama ziko hivo leo Ngara kwa shule za msingi mwaka jana ni wilaya ya mwisho ndani ya mkoa wa Kagera kwa matokeo ya darsa la saba, imefelisha sana kidato cha sita na vile vile kidato cha nne halikadhalika darasa la nne na kidato cha pili ukilinganisha na wilaya zingine mkoa huu. Je, Mbunge aliahidi kuwapatia MITUNGI YA GESI (aliyowagawia leo kila shule) ili kuboresha elimu? Hivi hizi shule zilijengewa wanafunzi ama walimu kwani uwepo wa vitabu, umeme mashuleni na uhusishaji kwa wazazi wa wanafunzi ndivyo vingesaida na kumnufaisha mwanafunzi akiwa darasani. Kama nia ni kuboresha mazingira ya kufundishia, basi hizo jitihada zinufaishe wanafunzi na mazingira bora wanaposomea ili utendaji wa walimu uwe bora darasani na sio kuwa bora kwenye ulingo wa siasa ambapo wameagizwa wakamchukulie Mbunge fomu ya kuwania ubunge kwa awamu ijayo. Hawa walimu wakuu waliopokea gesi hawawezi kuwakilisha hisia za kisiasa za kila mwalimu aliepo wanapofundisha. Kutumia uhaba na umasikini uliopo kama njia ya kumsukumia mwalimu kwenye ulingo wa Siasa sio uungwana na nikinyume za taratibu za taaluma zetu na pengine za nchi yetu.
Tatu, Walimu wenzangu naumia kuona kizazi cha wasomi kinahadaiwa kwa vitu vidogo wanasahau mambo ya msingi kwa hatma yao na maisha yao. Hivi chakula, vinywaji na nauli ndiyo msingi wa uboreshaji wa maslahi ya watumishi wa serikali nchi hii?. Ama Mbunge majukumu yake ni yapi katika kuwatetea watumishi wa UMMA (including walimu?).
Natua kalamu yangu chini kwa kukiasa sana Chama cha Walimu Wilaya ya Ngara. Najua ni wana CCM wazuri karibia ofisi nzima ila rasilimali za chama hiki (CWT) ni za wanachama na na zinatumika kwa shughuli za chama sio zile za kisiasa.
Tupambane sana makamanda kazi iliyo mbele yetu bado ni nzito sana.
✍️By Mwl. John Vugabiba, Mwalimu Mkuu, Simu Mfukoni