Watu watatu wa mkoa wa Kayaza kaskazini mwa Burundi wamefungwa miaka 30 jela kwa kupanga njama ya kumuua kiongozi wa taifa.
Kulingana na chombo cha habari cha eneo cha Isanganiro, wakili wa eneo hilo aliagiza wapige mawe magari matatu jioni wakati wa ziara ya kiongozi wa taifa ya siku tatu eneo hilo.
Wanaume wawili na mwanamke mmoja wameshtakiwa na wote wamekanusha madai hayo na hakimu anasema mawe hayo yalitokea eneo la makaburi ambapo wote wanafanyakazi.
Washitakiwa wawili wanafanyakazi katika kampuni ya mafuta ya Egen mkoani humo na mwingine ni fundi wa magari wa eneo hilo.
Mkaazi wa eneo la Kayanza ameiambia BBC kwamba gari lililokuwa na vilipuzi lililipuka katika kituo cha usajili wa polisi cha Iraq eneo la Kayanza.
“Waliwaelezea kwamba wengine wao waliachiwa huru isipokuwa hao watatu ambao, mwananamke mmoja na na wanaume wawili ndio waliohukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani jana (Jumapili),” amesema.
“Wengi walikamatwa baada ya tukio hilo, wengine wakaachiliwa huru baadae lakini mwanamke mmoja na wanaume wawili walisalia gerezani na kushtakiwa Jumapili” – mkaazi wa Kayanza ameiambia BBC Great Lakes.
Katika kesi hiyo, mwendesha mashtaka wa eneo hilo anawashutumu kwa “kushindwa kutoa taarifa kwa idara ya usalama ya kiongozi wa taifa na washirika wake”.
Huku mwendesha mashtaka akiwa amependekeza kifungo cha miaka saba gerezani kwa kusababisha ukosefu wa usalama kwa rais, mahakama iliwapata na hatia ya kujaribu kumuua rais na kuwafunga kifungo cha miaka 30 gerezani, kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya eneo.
Recent Comments