MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amesema CCM haikubahatisha kumteua Dk John Magufuli kuwa mgombea urais; na kwamba ana imani baada ya uchaguzi mkuu, atakabidhi kijiti cha urais kwa Dk Magufuli.
Akizungumza wakati akiwakabidhi Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020, Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema ana uhakika Magufuli atachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano. Alisema ana imani ya ushindi huo kwa sababu mgombea wa chama hicho uteuzi wake umelenga kutokana na sifa zake na kukubalika kwa wananchi.
âTunataka rais anayeipenda nchi yake na wananchi, hatutaki rais maskini ila mali zake ziwe zinaeleweka alikozipata, hatutaki kuchukua mgombea mwenye makandokando ambayo ingetupa shida kumtetea mbele ya wananchi, badala ya kwenda kuomba kura,â alisema Kikwete.
Alisisitiza kuwa Dk Magufuli anafaa, kwani hata wakati wa kugombea alikuwa mnyonge, tofauti na wagombea wengine ambao walikuwa na mbwembwe nyingi na hata wapambe wake alikuwa ni dereva wake pamoja na msaidizi wake.
Alisema kundi la Dk Magufuli ni la Watanzania na akasema kuwa ana imani kuwa chini ya utawala wa mgombea huyo, nchi itakuwa salama kwani ni mtu wa uhakika anayependa maendeleo.
Kikwete pia alitoboa wazi kuwa katika baadhi ya ofisi za chama za wilaya, baadhi ya makatibu wa chama hicho, walikataa kumpatia wadhamini kutokana na maelekezo waliyokuwa wameyapata kutoka kwa baadhi ya wagombea, jambo ambalo lilimlazimu Dk Magufuli kwenda kwenye matawi ya wanachama.
Alitumia kampeni hiyo kuwapiga vijembe baadhi ya vigogo waliotangaza kuihama CCM na kwenda upinzani akiwemo mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa na mgombea mwenza Juma Duni Haji kuwa hawana sera, bali wanachofanya ni kutangaza sera za CCM na CUF.
âMgombea urais anatangaza sera za CCM ndio maana akasema wataisoma namba, huo ni wimbo wa TOT, mwingine anatangaza sera za CUF,â alisema Kikwete na kuongeza, âMwingine jana nimemsikia amehama anadai anafanya hivyo kuiimarisha CCM, mimi siwaelewi kabisa na hadi leo sijui kasema nini.â
Alisema mtu anayesema anaenda kuwasaidia kuunda serikali wapinzani ni kama anawadharau kwamba wao hawana uwezo wa kuongoza Serikali. âLakini wameyataka wenyewe na mkutano huu wa Dk Magufuli ni mfano kuwa CCM ina watu na picha hizi ndizo halisi sio zile za kuunganisha.â
Recent Comments